Ticker

6/recent/ticker-posts

HAZINA SPORT YAIBUKA MSHINDI DHIDI YA IKULU NA CHUO CHA IRDP


Mgeni rasmi wa Bonanza la Michezo kati ya Hazina, Ikulu na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini ambaye ni Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Hozen Mayaya, akifunga michezo hiyo, jijini Dodoma.


Mgeni rasmi wa Bonanza la Michezo kati ya Hazina, Ikulu na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini ambaye ni Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Hozen Mayaya, akipeana mkono na wachezaji wa Hazina, wakati wa bonanza la michezo hiyo, jijini Dodoma.


Kapteni wa Hazina Sport Club, Bw. Mgusi Msita, akiuondoa mpira eneo la hatari, wakati wa mchezo kati yao na Ikulu, katika viwanja vya Kilimani, jijini Dodoma.


Kikosi cha timu ya Hazina wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mtanange na wanamichezo wa Ikulu, katika viwanja vya Kilimani, jijini Dodoma.


Kikosi cha timu ya Hazina wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mtanange na wanamichezo wa Chuo cha Mipango, katika viwanja vya Kilimani, jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma)

************************

Na. Peter Haule, WFM, Dodoma

Hazina Sport Club imeibuka mshindi wa jumla katika michezo ya mpira wa miguu, kuvuta kamba na mpira wa pete dhidi ya timu ya Ikulu na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) Dodoma.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Hazina Sport Club, Bw. Mgusi Msita, wakati wa Bonanza la michezo kati ya Hazina, Ikulu na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) Dodoma lililofanyika katika viwanja vya Kilimani, iliyolenga kujenga afya, udugu na ushirikiano katika kulitumikia Taifa.

Bw. Msita alisema kuwa timu ya michezo ya Hazina ni washindi wa jumla kati ya timu tatu ambapo katika mpira wa miguu Hazina imeshinda goli mbili kwa sifuri dhidi ya Ikulu na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Dodoma.

Katika mchezo wa kamba kwa upande wa wanaume Hazina imeibuka mshindi dhidi ya Ikulu lakini imepoteza dhidi ya Chuo cha Mipango ili hali kwa upande wa wanawake Hazina imeibuka mshindi dhidi ya Chuo cha Mipango.

Pia katika mchezo wa mpira wa pete Hazina imeibuka mshindi kwa kupata vikapu 75 ilihali Chuo cha Mipango kikiambulia vikapu 25 pekee.

Bw. Msita alisema kuwa michezo inajenga afya ya mtumishi mmoja mmoja na humsaidia mtumishi wa umma kufanya kazi kwa ufanisi katika kuwatumikia wananchi lakini pia inajenga ushirikiano na uhusiano wa kikazi ndani na nje ya taasisi, ikizingatiwa bonanza hilo limehusisha taasisi tatu.

Awali mgeni rasmi wa Bonanza na Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), Prof. Hozen Mayaya, aliipongeza Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuandaa bonanza hilo ambalo linasaidia katika kuimarisha afya ya akili na kuwataka wanamichezo wakiwemo Ikulu na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, kuandaa michezo hiyo mara kwa mara ili kuweza kuimarisha zaidi ushirikiano na kujenga Afya.

Post a Comment

0 Comments