Ticker

6/recent/ticker-posts

MAADHIMISHO YA SIKU YA KISWAHILI DUNIANI: MRISHO MPOTO KUPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA NCHINI UFARANSA

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Mohamed Mchengerwa akimkabidhi bendera ya Tanzania msanii Mrisho Mpoto ambaye anakwenda nchini Ufaransa katika Maadhimisho ya Siku ya Kiswahi Duniani ambayo yatafanyika nchini Ufaransa Julai7, 2022. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Mohamed Mchengerwa akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 5,2022 Jijini Dar es Salaam wakati akimkabidhi bendera ya Tanzania Msanii Mrisho Mpoto ambaye anaenda kuiwakirisha Tanzania katika Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani nchini Ufaransa.
Msanii Mrisho Mpoto akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 5,2022 Jijini Dar es Salaam mara baada ya kukabidhiwa bendera wakatti akijiandaa na safari ya kuelekea nchini Ufaransa kwenye maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani ambayo yatafanyika Julai 7,2022.

*************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SERIKALI kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo leo Julai ,2022 imemkabidhi bendera ya Taifa Msanii Mrisho Mpoto kwaajili ya kwenda kushiriki maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani nchini Ufaransa.

Mrisho Mpoto alipokea mwaliko kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa (UNESCO) na Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania, maadhimisho hayo yatafanyika Julai 7,2022 katika makao makuu ya UNESCO nchini Ufaransa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Mohamed Mchengerwa amempongeza Mrisho Mpoto kwa kwa kazi kubwa ambayo anaifanya kwa kutumia sanaa yake kukuza Utamaduni wa Kitanzania hususan matumizi sahihi ya ya lugha ya Kiswahili katika tungo zake.

"Nitoe rai kwa wasanii wengine kuiga mfano wa Mpoto katika sanaa zao , sanaa ni kioo cha jamii, sanaa inapaswa kuburudisha jamii, kuiendeleza jamii, Sanaa si matusi na si ugomvi wala mambo yasiyo na stala , na kwa kufanya hayo Mpoto asingepata fursa hii ya kwenda Ufaransa". Amesema Waziri Mchengerwa.

Kwa upande wake Mrisho Mpoto amesema kuna umuhimu mkubwa kwa watanzania kuendelea kuitanggaza lugha ya Kiswahili ulimwenguni kwa maana kuna baadhi ya nchi za wenzetu hawafahamu yakuwa lugha mama ya watanzania ni Kiswahili, ifikie kipindi sasa wafahamu yakuwa Kiswahili kinazungumzwa Tanzania.

Post a Comment

0 Comments