Ticker

6/recent/ticker-posts

MJUMBE WA NEC SINGIDA AWAHIMIZA WANANCHI KUSHIRIKI SENSA

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Mkoa wa Singida, Yohana Msita akionesha fomu ya kugombea nafasi hiyo kwa kipindi kingine tena katika mchakato wa kupokea na kurudisha fomu kwa wanachama wa chama hicho ulioanza jana mjini hapa.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Mkoa wa Singida, Yohana Msita akisubiri kukabidhiwa fomu hizo.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Mkoa wa Singida, Yohana Msita akijaza fomu hizo na baadae kuzikabidhiwa kwa ajili ya hatua nyingine.








*********************

Na Dotto Mwaibale, Singida




WANANCHI Mkoa wa Singida wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litaklofanyika Agosti 23, 2022.

Ombe hilo limetolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Mkoa wa Singida, Yohana Msita wakati akirudisha fomu ya kugombea nafasi hiyo kwa kipindi kingine tena katika mchakato wa kupokea na kurudisha fomu kwa wanachama wa chama hicho ulioanza jana.

"Nitumie nafasi hii kuwaomba wananchi wote mkoani hapa kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi na kutoa ushirikiano kwa maofisa watakuwa kuwa wakifanya kazi hiyo" alisema Msita.

Akizungumzia Umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 Msita alisema ni pamoja na kuisadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa.

Alisema taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya juu ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali na kupata taarifa za msingi za hali ya kidemografia, kijamii na kiuchumi za idadi ya watu na makazi za mipango kwenye ngazi zote.

Aidha Msita alisema umuhimu wa sensa hiyo ni pamoja na kigawio katika kukokotoa viashiria vingine mfano Pato la mtu mmoja mmoja, Pato la Taifa, Ajira na ukosefu wa Ajira na kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi.

Pia alisema umuhimu wa sensa hiyo ni kupata taarifa itakayowezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira na msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia.

Alisema Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi, kurekebisha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa na maeneo mengine.

Msita alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi ambazo zimetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani hapa ambapo kwa mwaka mmoja tangu awe madarakani mkoa wa Singida ulipatiwa Sh.230 Bilioni.

Post a Comment

0 Comments