Ticker

6/recent/ticker-posts

SHEKIFU ASEMA VYAMA PINZANI VIMESAIDIA CCM KUIMARISHA MKOA WA TANGA


Katibu Msaidizi wa Ccm Mkoa wa Tanga Kumotola Kumotola akimpa maelekezo Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Tanga Henry Shekifu wakati aliporudisha fomu ya kugombea nafasi hiyo, kushoto ni Katibu wa Ccm Mkoa huo Suleimani Mzee Charasi.




Mwenyekiti Henry Shekifu kulia akikabidhi fomu yake kwa Katibu Suleimani Mzee Charasi.




*******************


Na Hamida Kamchalla, TANGA.


USHIRIKISHWAJI mzuri wa Vyama vya siasa Mkoa wa Tanga umechangia kuleta amani na ukuaji wa siasa ikiwa ni moja kati msingi uliowekwa na Chama cha Mapinduzi (Ccm) mkoani humo.


Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Tanga ambaye amemaliza muda wake, Henry Shekifu wakati akichukua fomu ya kugombea na kutetea kiti chake.


Akiongea baada ya kuchukua fomu hiyo Shekifu amesema Mkoa una mahusiano mazuri na vyama vya upinzani na umeimarika hakuna tena uadui kwakuwa wanawashirikisha katika ia vukao ambavyo vinawahusu.


"Mkoa wa Tanga tuna mahusiano mazuri na vyama vingine, hilo ndilo lililotufikisha hapa, tunajitetea kwa sera na utekelezaji mzuri, maadui wameondoka wenyewe na sasa tumeinarika na kuwa kitu kimoja" amesema Shekifu.


"Kwahiyo mimi nasema, maswala ya kuzungumza na wapinzani ni jambo la msingi, hawa wanatuimarisha wanaweza wakakwambia hapa una doa hakwambii kwa ubaya ila ni kwa upendo, sisi siku zote tunawakaribisha kwenye vikao vyote ambavyo vinawahusu watu wote tunawashirikisha" amebainisha.


Aidha Shekifu alisema ameamua kutetea kiti chake kwakuwa anajiona bado ana haki na uwezo wa kusimamia majukumu ya chama na tayari ameshaweka mahusiano mazuri ndani ya chama hicho.


"Nimechukua fomu kwa ajili ya kutetea nafasi yangu ya mwenyekiti Ccm Mkoa, nimeweza kukaa na wanachama na viongozi wenzangu, mwanzoni kabisa tulianza kujenga msingi wa chama kwa kuhakikisha hali inakuwa salama Tanga" amesema.


"Lakini pia tumeweza kushikamana Mkoa umetulia na watu wameimarika kichama vlevile tumeondoa zile figisufigisu zilizokuwepo za watu kukatwa majina yao, na hii imetuongezea upendo sana ndani ya chama" amefafanua Shekifu.


"Nimeona nilipofika siyo pabaya, bado nina nguvu za kuweza kusaidia kutoa mawazo, kusimamia utekelezaji na bahati nzuri nina watendaji wazuri ambao wanafanya kazi zao vizuri, sasa tunayo maeneo tunayohitaji kusimamia kwa mkakati mziti sana, bila kuwepo na uongozi imara tutayumba" amesema.


Hata hivyo alibainisha kwamba umoja uliopo umewajengea heshima kubwa na ili kuweza kutaendeleza hayo wanalenga mbele ifikapo mwaka 2025 chama kinahitajika kujiweka sawa na kutokujenga mambo ambayo yataleta makundi.


"Tumeondoa majungu tumeweka mshikamano na undugu, haya ndiyo ya kuyasimamia ili chama kiimarike, na mimi nasema kwa umri wangu sasa nasimamia ili nipate cha kuacha kama kumbukumbu, na kipindi kijacho nitaacha kumbukumbu na tutawapa nafasi vijana na wao wasimamie ili tupate uongozi bora" amefafanua

Post a Comment

0 Comments