Ticker

6/recent/ticker-posts

TEMDO YASHAURI WENYE VITUO VYA AFYA KUTEMBELEA OFISI ZAO KUPATA VIFAA TIBA VILIVYO BORA

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Dkt.Sigisbert Mmasi akiwaelezea namna vitanda walivyovitengeneza kwaajili ya kutumika hospitali baadhi ya wananchi waliotembelea banda la TEMDO katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

***************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) imewashauri wenye hospitali na vituo vya afya watembelee TEMDO ili waweze kupata vifaa tiba vya hospitali vilivyobora na kuthibitishwa na TMDA pamoja na MSD.

Ushauri huo umetolewa leo Julai 2,2022 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko TEMDO, Dkt.Sigisbert Mmasi katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam

Amesema umuhimu wa vifaa ambavyo wanatengeneza vinakuwa tofauti na viile vifaa vinavyotoka nje ya nchi kwasababu unavyotengeneza kifaa au mashine wanahakikisha inaendana na uhalisia tofauti na vifaa vinavyoka nje ya nchi.

Amesema katika Maonesho hayo wamekuja na vitanda kwaajili ya daktari kumkagulia mgonjwa, vitanda kwaajili ya kujifungulia wakina mama wajawazito pia wanakitanda kwaajili ya kutumika kuwalazia wagonjwa.

Aidha Dkt.Mmasi amesema licha kuweza kutengeneza kitanda kwaajili ya wagonjwa pia wametengeneza kiteketezi kwaajili ya kuchoma taka ngumu hatarishi za hospitali kilicho bora na ubunifu wake ni wa hali ya juu ambapo inachoma mpaka nyuzi joto 1200.

"Taka za hospitali ukizichoma kwa nyuzi joto ndogo zinakuwa hataishi zaidi lakini ukizichoma kwenye nyuzi joto 1200 na kuendeleza zinakuwa sio hatarishi". Amesema Dkt.Mmasi.

Ameeleza kuwa kifaa hicho ambacho kinatumika kuchoma taka hospitali kishapimwa na kuonekana kwamba uchafu unaotokea juu (moshi) hauna madhara yoyote katika mazingira.

Post a Comment

0 Comments