Ticker

6/recent/ticker-posts

VETA CHANG'OMBE YAGUNDUA DAWA ASILI YA KUUA WADUDU KWENYE MAZAO



**********

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Chang’ombe imegudua dawa za asili ya kupulizia na kuua wadudu na kuondoa magugu shambani

Akizungumzakatika maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba), Mwalimu wa Chuo cha VETA Chang’ombe, Ally Issa amesema, katika kukabiliana na wadudu waharibifu mashambani wameamua kubuni dawa hiyo ya asili ambayo itaweza kuondoa chagamoto inayowakumba mashambani wakulima.


"Wakulima wamekuwa na changamoto mbalimbali katika kilimo ikiwemo ya kuharibika kwa mazao mashambani, hivyo kupitia dawa hii ya asili ya wataweza kupuliza na kuua wadudu na kuondoa magugu shambani,"amesema.


Amesema, dawa hiyo ni mkombozi kwa wakulima na inapatikana kwa urahisi kwani imebuniwa na wazawa kutoka VETA.


Ameongeza kuwa, dawa hiyo ipo katika uangalizi na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) katika hatua ya mwisho wakiwa wamepata cheti cha uchunguzi na kibali cha muda cha maonesho ikiwa tayari itaingia sokoni

Post a Comment

0 Comments