Ticker

6/recent/ticker-posts

VIJANA MNAONENDA KUSOMA NJE YA NCHI MTUMIE FURSA YA KURUDI NA WAWEKEZAJI SIO VYETI PEKE YAKE


Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Kampuni Global Education Link Abdumalik Mollel akiwa na Timu yake ishara ya wakiwa wamesimama Wakati Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa akitembelea mabanda mengine na kupita banda lao kiwapungia mkono Waandishi wa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Kampuni Global Education Link Abdumalik Mollel akizungumza na Waandishi wa habari katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Mabanda ya Maonyesho ya Global Link katika Viwanja vya Mnazi Mmoja
Wakala wa Kampuni ya Global Link akihudimia Mteja.


*********

Na Magrethy Katengu

Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Kampuni Global Education Link Abdumalik Mollel amewashauri Wanafunzi wanaoenda kusoma nje ya nchi wahakikishe wanatumia fursa hiyo vizuri siyo kurudi na cheti peke yake bali warudi na wawekezaji ili kusaidia Taifa kuondokana na tatizo la ajira na Uchumi wa nchi kuimarika zaidi na zaidi.

Ushauri huo ameutoa leo Dar es salam wakati akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa kufunguzi wa Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu,Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa Wizara ya Elimu Sayansi na teknolojia kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU) yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

"Kampuni ya Education Link tumeona tuvilete Vyuo Vikuu vya Ulaya hapa kwenye maonesho ili kuwasaidia vijana kuomba kwenda kusoma kwenye nchi hizo, lengo letu siyo wanafunzi wanaenda kusoma nje ya nchi warudi na chetu tu bali tunataka warudi na wawekezaji kuleta fursa ya Uwekezaji nakutusaidia kuajiri vijana wenzao kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira" Amesema Mollel.

Sanjari na hayo Mollel amesema Vijana hukukosa ufadhili wa nafasi za masomo nje ya nchi kutokana na changamoto ya kuchelewa kutuma maombi British Council na waliowengi hupelekea maombi tarehe za mwishoni hivyo waombaji kuwa wachache hivyo kupitia maonyesho hayo wanawapatia elimu wamekuja kitofauti kuwasaidia vijana wote wanahitaji ufadhili wa kusoma nje ya nchi .

"Wanafunzi wa Tanzania wanaohitaji kusoma chuo chochote nje ya nchi ikiwemo Uturuki ambapo vipo zaidi ya 40 hapa katika kozi za Sayansi, afya,biashara,Sanaa pia nchi Saipras India, Georgia iliyoko bara la Umoja wa Ulaya sisi tu wawakilishi wao hivyo Wazazi walezi wanaotamani vijana wao kusoma nje ya nchi wawalete"alisema Mollel

Hata hivyo Abdumalik Mollel amewashauri wanafunzi wanaotaka kujiunga na Vyuo Vikuu vya nje ya nchi wachangamkie fursa katika nchi za Umoja wa Ulaya ikiwemo Georgia na Cyprus kwani nchi hizo zina fursa ya kupata ajira kwa urahisi, na wawekezaji kutokana na kuwa na idadi ndogo ya nguvu kazi ya Taifa ambao ni vijana huku wazee wakiwa wengi.

"Nchi Georgia ina idadi ya watu takribani milioni nne, huku wazee wakiwa wengi kuliko vijana hivyo inakabiliwa changamoto ya nguvu kazi Taifa kutokana nakuwa na idadi ndogo ya vijana hivyo wanafunzi kutoka mataifa mengine ambao wanaenda kusoma kwenye nchi hiyo wanaweza kupata ajira kirahisi baada ya kuhitimu masomo yao na kutangaza fursa za nchi zao kuvutia wawekezaji "alisema Mkurugenzi

Mkurugenzi amebainisha kuwa wanafunzi wanaosoma kwenye nchi hizo za Ulaya wanaweza kupata Visa ya Shengen ambayo inawapa fursa ya kuzunguka nchi zipatazo 30 ikiwemo Italia, Ujerumani, Ufaransa, Hungary na Poland ambapo nchi hizo ni kubwa zenye teknolojia kubwa lakini pia zina changamoto ya idadi ya watu hivyo zinahitaji nguvu kazi.

Kwa upande wake, Meneja wa Kitengo cha Mitihani kutoka British Council-Tanzania, Henry Sangilwa amesema kuwa lengo la kuja kwenye maonesho hayo ni kuwaletea Vijana wa kitanzania habari njema za fursa za ufadhili wa masomo zinazopatikana Nchini Uingereza.

"Kila mwaka tumekuwa tukitoa nafasi za ufadhili zipatazo 35 za wanafunzi kwenda kusoma nje ya nchini lakini cha kushangaza ni wachache wanaonufaika sababu ni wengi kukosa taarifa sahihi kwa wakati hivyo huja kufanya maombi wakati muda ukiwa umekwisha hivyo mwaka huu nawasisitiza tunafungua dirisha Agosti hadi Novemba kwa daraja la (Master digree) hivyo wajitokeze wasiogope mitihani ni ya kawaida tu

Post a Comment

0 Comments