Ticker

6/recent/ticker-posts

WANAHABARI WAPEWA KONGOLE KWA KAZI NZURI YA KUUHABARISHA UMMA



***************************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.


WAANDISHI pamoja na Vyombo vya habari nchini wamepongezwa kwa kazi nzuri wanazofanya kwa kuuhabarisha umma hasa katika kipindi hiki kinachoendea kwenye Sensa ya Watu na Makazi inayotarajia kufanyika Agosti 23 mwaka huu.

Akiongea kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima, katika ufungaji wa mafunzo ya wakufunzi wa sensa ngazi Mkoa, mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashimu Mgandilwa amesema wanahabari wamekuwa mstari wa mbele katika kuuhabarisha umma kuhusiana na jambo kubwa na la kipekee nchini.

"Ndugu zangu wa vyombo vya habari wakati wote vimekuwa chachu katika kuchagiza maendeleo ya nchi yetu, hivyo katika hili la kutoa elimu ya sensa, tuzidi kuvionba viendelee kufanya hivyo hadi tutakapokamilisha jambo hili la sensa ambalo tunatarajia kulifanya" alisema.

Mgandilwa amesema mafunzo waliyopatiwa washiriki hao kwa ngazi ya Mkoa, yalitanguliwa na mafunzo kama hayohayo kwa ngazi ya Taifa ambayo lengo kubwa ni kuwafundisha wakufunzi ambao kwa mamma moja au nyingine mao wanawafundisha wakufunzi hao wa ngazi za Mkoa.

Amesema baada ya mafunzo hayo ya siku 21 waliyopatiwa wahitimu hao, watakwenda kuwafundisha makarani na wasimamizi wa sensa katika ngazi ya Wilaya kuanzia siku ya ijumaa julai 29, na kuongeza kuwa mafunzo hayo yalikuwa na umuhimu wa kipekee katika kuifanikisha sensa katika katika Mkoa wa Tanga.


"Nasema hivyo kwakuwa haya ndio mafunzo mama ambayo yatatumika katika kujenga msingi bora na imara wa mafunzo mengine katika ngazi ya Wilaya, kupitia hili na uwepo wenu katika mafunzo haya kumenifanya nipitie mara kwa mara kuona mchakato mzima toka mnaanza mpaka cku ya leo" alisema.


"Sote tunafahamu kwamba sensa ya watu na makazi ni muhimu kwa Taifa letu, Kikanda na Kimataifa, itatuwezesha kupata takwimu muhimu zitakazosaidia kupanga, kupima na kutathmini utekelezaji wa mipango yetu mbalimbali ya kimaendeleo" alibainisha.


Aidha ametoa shukurani na pongezi kwa waandaaji waliofanya uchambuzi wa kuwahusisha watu wenye mahitaji maalumu kwakuwa haitokei mara kwa mara makundi ya watu hao hawashirikishwi katika maswala muhimu katika jamii.


"Naomba niwapongeze pia waandaaji na wachambuzi wote, kipekee ni bahati kwamba iliyipo, kwenye kundi letu wapo watu wenye mahitaji maalumu ambao wapo kwenye maeneo yetu, ni nadra sana kukuta wanashirikishwa, lakini tuliona tuna kila sababu kwakuwa kuna maeneo wanaweza kutusaidia" alisema.


Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Arbogast Kimasa amesema Mkoa ulikuwa na tatizo la wananchi kutokea na elimu ya uelewa kuhusu sensa kwakuwa hamasa inaonekana kuwa ngazi za juu na kwamba elimu hiyo haikuwafikia wananchi na tathmini ikaonesha Mkoa wa Tanga unavuta mkia.


"Sasa kwa maana takwimu hizi zinatumia tehama na sisi tulipimwa kwa tehama nina imani baada ya mafunzo haya, sensa itaongoza Mkoa wa Tanga, hapo mwanzo wale watu walikuwa wanaulizwa kwa kutumia simu, wakasema sensa Tanga haijulikani" alisema Kimasa


"Ile historia iliyofanyika mwezi Juni, ikifanyika tena mwezi Agosti mwanzo, basi ibadilishe zile takwimu na ionekane sisi Tanga watu wanaelewa kwasababu washiriki wote kutoka kila halmashauri ni watu wa kutimua vumbi,


"Maana yake sisi hatuvuti mkia Bali tunaongoza kwa kila kitu, kuanzia halmashauri, mapato na sasa tuoneshe kama hamasa hii itafanya kazi kwa wale tunaowapa majukumu kwenye Wilaya, kata na vijijini ili sensa iwe ya mafanikio" alisisitiza.

Post a Comment

0 Comments