Ticker

6/recent/ticker-posts

WATUHUMIWA 2 MBARONI KWA TUHUMA ZA MAUAJI



*********************

Na Magrethy Katengu

JESHI la Polisi Kanda Maalumu Dar es salaam linawashikilia watuhumiwa 2kwa tuhuma za Mauaji 8 Wizi wa kuvunja majumbani kwa kutumia silaha ikiwemo Panga bisibisi.

Akizungumza na Waandishi wa habari Kamanda Jumanne Muliro amesema katika tukio la kwanza linamshikilia Selemani Haruna @Kwata umri24 mkazi wa Kimara Temboni mtaa wa Amani, kwa tuhuma za kumuua Editha Charles miaka 22 Binti wa kazi za ndani na kuuficha mwili wake katika stoo ya vifaa vya ujenzi nyumba ya Agatha Stanslaus ambaye ni bosi wa Binti huyo.

Kamanda amesema Uchunguzi wa awali uliofanyika umeonesha mtuhumiwa Julai 6 mwaka huu majira ya asubuhi alifika kwenye nyumba aliyokuwa anayoishi binti huyo akijifanya fundi wa umeme kwamba alitakiwa kuweka balbu alipoingia alimshambulia kwa kitu chenye ncha kali binti huyo na kumuua halafu akavunja chumba cha mwenye nyumba na kuiba pesa TZS 1,800,000/= na kutoweka.

"Polisi kwa kutumia wataalamu wake wa uchunguzi wa kisayansi na vyanzo vingine vya kiuchunguzi walibaini mtuhumiwa huyo kuwa aliingia kwenye nyumba hiyo na kukaa kwa masaa kadhaa na kutoka baada ya kumkamata na kumhoji kwa kina alikiri kumuua binti huyo, kuvunja mlango wa chumba na kuiba pesa Tsh 1,800,000/= na Mwili wa marehemu aliuficha kwenye stoo ya nyumba hiyo huku akiwa ameufunika na vifaa mbalimbali vya ujenzi ili usionekane." alisema Kamanda

Hata hivyo Jeshi la Polisi walimsachi na alionesha kiasi cha pesa alizoziiba eneo hilo na pesa zingine alidai mara baada ya tukio siku iliyofuata alinunua vitu mbalimbali zikiwemo simu mpya aina ya Infinix, viatu vya mpira pea 2, na begi la mgongoni lenye nguo mbalimbali mpya ambavyo navyo vimepatikana.

"Kwa kweli kiitendo alichofanya mtuhumiwa ni cha ukatili uliopita kiasi, uchunguzi wa shauri hili unakamilishwa na atafikishwa katika mifumo ya kisheria ikiwa ni pamoja na Mahakamani haraka iwezekanavyo " Alisema Muliro

Katika tukio lingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linamshikilia Jonas Ziganyige umri 71mtaafu wa Jeshi la Wananchi, Mkazi wa Mbezi juu kwa tuhuma za kumpiga risasi na kumuua Patient Romwadi umri 48 mfanyabiashara Mkazi wa Wazo Mivumoni, Kinondoni.

Kamanda alisema taarifa za awali, zinaonesha kuwa Julai 9 Mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi Recy Renso umri 52 mkazi wa Posta alifika eneo hilo na mtu huyo ambaye ni marehemu kwa sasa kwa lengo la kuangalia mipaka ya kiwanja chake ghafla Mtuhumiwa alitoka ndani huku akionesha kukasirishwa na hatua ya watu hao, akachukua bunduki na kumpiga risasi Patient Romward ambaye baadae alifariki.

Baada ya tukio hilo mtuhumiwa alikimbia lakini upelelezi ulifanywa haraka na Julai 10 mwaka huu alikamatwa eneo la Kibaha Maili Moja akiwa amejificha na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam pia limeipata silaha aliyotumia mtuhumiwa ambayo ni aina ya Mark IV ikiwa na risasi 4. Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo kujibu mashtaka yanayo mkabili.

Sanjari na hayo Jeshi la Polisi Kanda maalum linaendelea pia na jitihada za kuzuia vitendo vya kihalifu kwa kufanya Oparesheni kali inayoongozwa na taarifa dhidi ya Uhalifu na Wahalifu katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam. Watuhumiwa 8 sugu wa uvunjaji nyumba na kuiba vifaa vya magari akiwemo Jumanne Omary umri28 mkazi wa Mikwambe na wenzake 7 wamekamatwa wakiwa na Tv flat screen za aina ya mbalimbali 4, laptop mbili, sab ufa moja, simu aina mbalimbali tano pamoja na vifaa vya kutendea uhalifu vikiwemo mikasi miwili mikubwa ya kuvunjia, panga moja, kisu kimoja, Prize na Bisibisi, Tochi na Nyaraka mbalimbali .

Pia gari lenye namba za usajili T.787 DGW aina ya Toyota Gaia limekamatwa kwa kuhusishwa na kutumiwa kwenye vitendo vya kihalifu.

Aidha Jeshi la Polisi Kanda Maaluma ya Dar es salaam linatoa wito kwa wananchi kuacha kujihusisha na vitendo vya kihalifu kwani kwa kufanya vitendo hivyo watakamatwa na watajikuta wakiwa katika msuguano mkali wa kiseria na vyombo vya dola.

Post a Comment

0 Comments