Ticker

6/recent/ticker-posts

ADC YAUNGANA NA SERIKALI KUHAMASISHA SENSA

Mwenyekiti wa Chama cha ADC Hamadi Rashidi akizungumza na waandishi wa habari
Katibu Mkuu wa chama cha ADC Doyo Hassan Doyo akizungumza na waandishi wa habari 

****************

Na Magrethy Katengu

Chama cha Allience Democratic for change kimewashauri Wananchi kuachana na udini,ukabila uchama katika tukio kubwa la Kitaifa linalotarajiwa kufanyika 23 Agosti mwaka huu la Sensa.

Ushauri huo ulitolewa leo Dar es salaam na Mwenyekiti wa Chama cha ADC Hamadi Rashidi wakati wa ufunguzi wa warsha ya uelimishaji wananchi kuhusu umuhimu wa sensa ambapo amesema ili nchi iweze kujiendesha na kupanaga mipango ya maendeleo vizuri ni lazima kuwe na takwimu sahihi za watu.

Mhe. Hamad amesema hali ya uchumi Sasa si rafiki kwa maisha halisi ya Mtanzania kwani bei za bidhaa zinazidi kupanda bei hivyo kupitia zoezi hilo la kuhesabu watu serikali inaweza kutathimini namna ya kusaidia kupunguza makali Kwa kutoa fedha kwanza lazima ijulikane idadi sahihi ya wananchi waliopo.

Sambamba na hayo amesema hivi karibuni bei ya mafuta imepanda tena kwa kuongeza uagizaji mafuta kwa wingi yatakayotumika Kwa Muda mrefu Ili kusaidia hata kama bei ikiongezeka kunakuwa unafuu kidogo.

Sanjari na hayo amesema Maendeleo ya Makubwa yanategemea Sensa kwani ugawaji wa Vijiji,Wilaya,Mkoa inategemea na sensa Ili kusaidia serikali katika upekekaji wa huduma za kijamii ikiwemo maji,hospitali,hospitali,Barabara huduma zote hizo lazima ingaliwe idadi ya watu.

"Kuna baadhi ya watu wamekuwa na Mila potofu za kujataa kuhesabiwa baadae huduma za kijamii zinapoletwa hazikidi idadi yao wanakuwa kipaumbele kulalamika kumbe sababu ni wao wenyewe hivyo niwatake badilikeni jitokezeni muhesabiwe"amesema Rashid

Naye Katibu Mkuu wa chama cha ADC Doyo Hassan Doyo amesema Hadi kufikia Agosti 23 mwaka huu watahamikisha wamezunguka Mikoa yote nchini kulingana na serikali kuhamasisha Sensa kwani nao wanahusika zaidi kutokana na Mlengo wao wa kushika Dola ifikapo 2025 lazima wakishika uongozi watambue idadi ya watu wanaowaongoza.

"Maafisa wa sensa nawashauri kwenye zoezi la dodoso muwe wakarimu wapole na lugha nzuri wanyenyekevu muendane na tabia za watu kwani mkienda kichwakichwa mnaweza msipate takwimu sahihi kwani siyo wananchi wote wenye mwitikio wa kuhesabiwa wengine bado hawana elimu ya kitosha juu ya sensa"amesema Doyo

"Mratibu wa Taifa Sensa usikubali kwenye maeneo ya zoezi la sensa kuwa na Wageni ambao hawafahamiki katika eneo husika kuchukua takwimu za watu kwani kunaweza kutolea mkwamo Kwa kupata upinzani mkubwa kwani wengine hupenda kuteta kwa lugha zao kutoa takwimu zisizo sahii"amesema Doyo

Aidha chama cha ALLIANCE for Democratic change ADC kinatoa wito kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla kujitoka kuhesabiwa katika zoezi sensa Agost 23 mwaka huu na kuondoa dhana za kizamani kuwa kuhesabiwa ni mikosi.

Post a Comment

0 Comments