Ticker

6/recent/ticker-posts

BoT YAHIMIZWA KUHAMASISHA WANANCHI KUWEKEZA KATIKA DHAMANA ZA SERIKALI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Gavana wa BoT, Sera za Uchumi na Fedha, Dkt. Yamungu Kayandabila, alipofika katika banda la BoT kwenye Maonesho ya Wakulima ya Nanenane kwa ajili ya kuzindua Mpango wa Serikali wa Kushirikisha Vijana katika Kilimo Biashara.

*************************

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Yamungu Kayandabila, ameitaka BoT kuongeza uhamasishaji kwa wananchi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, pamoja na shughuli zingine za kilimo, kuwekeza katika dhamana za serikali.

Dkt. Kayandabila aliyasema hayo alipotembelea banda la BoT katika Maonesho ya Wakulima - Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya mapema leo.

“Hamasisheni zaidi wananchi wa Kanda ya Nyanja za Juu Kusini kuwekeza katika dhamana za Serikali,” alisema Naibu Gavana wakati alipotembelea meza ya Masoko ya Fedha, ambapo alielezwa kwamba wananchi wamekuwa wakifika kupata elimu kuhusu uwekezaji katika dhamana za serikali.

Dkt. Kayandabila pia aliagiza kuongezwa kwa matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika kutoa elimu kwa wananchi ili kurahisisha uelewa badala ya maelezo pekee.

Akiwa katika meza ya Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi katika banda hilo la BoT, Naibu Gavana aliagiza takwimu za bei za mafuta katika soko la duni kuchakatwa na kutoa matarajio kwa wananchi kuhusu bei za bidhaa hiyo muhimu katika siku za usoni.

“Angalia takwimu za mafuta kwa kipindi cha miezi na wiki kadha. Toa matumaini kwa wananchi kuhusu mwelekeo wa bei hizo kwa siku za usoni,” alisema Dkt. Kayandibila.

Kuhusu masuala ya mifumo ya malipo ya taifa, Naibu Gavana ameitaka Benki Kuu kufanya kazi na wadau wengine, ikiwemo Wizara ya Fedha na Mipango ili kupunguza malalamiko ya wananchi ambayo yanajitokeza mara kwa mara.

Benki Kuu ya Tanzania inashiriki katika Maonesho ya Nanenane kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo utafiti na sera za uchumi, namna ya kuwekeza katika dhamana za serikali, namna BoT inavyosimamia mifumo ya malipo ya taifa na sekta ya fedha nchini, Bodi ya Bima ya Amana, Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania, namna dawati la kutatua malalamiko ya wateja za mabenki linavyofanya kazi pamoja na elimu ya utambuzi wa alama za usalama katika noti zetu.

Naibu Gavana, Dkt. Yamungu Kayandabila, akipewa maelezo na Kaimu Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, Bi. Victoria Msina, kuhusu huduma zinazotolewa katika banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Mbeya.

Meneja Idara ya Sarafu BoT, Bw. Ilulu Ilulu, akielezea alama za usalama zilizopo katika sarafu ya shilingi 500 kwa Naibu Gavana, Sera za Uchumi na Fedha BoT, Dkt. Yamungu Kayandabila (wa pili kutoka kushoto) alipotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Mbeya. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji BoT, Bw, Kened Nyoni, Kaimu Meneja, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki BoT, Bi. Victoria Msina na Afisa Uhusiano wa Umma na Itifaki, Bi. Beatrice Ollotu.

Naibu Gavana, Dkt. Yamungu Kayandabila, akifafanua jambo kuhusu sekta ya fedha kwa wakaguzi wa mabenki alipotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane jijiini Mbeya. Kushoto ni Mkaguzi wa Mabenki Mwandamizi, Bw. Gwamaka Charles, Afisa Sheria BoT, Bw. Ramadhani Myonga na Afisa kutoka Bodi ya Bima ya Amana (DIB), Bi. Joyce Shala.

Naibu Gavana, Dkt. Yamungu Kayandabila, akizungumza jambo na Afisa Mkuu Mwandamizi wa Benki, Bi. Joyce Njau, kuhusu usimamizi wa mifumo ya malipo ya taifa. Wengine ni Kaimu Meneja, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki BoT, Bi. Victoria Msina, Afisa Rasimali Watu Mwandamizi, Bi. Consolata Shao na Bw. Maximilian Kishiwa.

Naibu Gavana, Dkt. Yamungu Kayandabila, akielezea jambo kuhusu dhamana za serikali alipotembelea banda la BoT katika Maonesho ya Nanenane. Katikati ni Mchambuzi Mkuu wa Masuala ya Fedha BoT, Bw. Ephraim Madembwe na Bw. Hassan Mbaga.

Naibu Gavana, Dkt. Yamungu Kayandabila, akizungumza na wachumi katika banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane. Kutokea kulia ni Mkurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji BoT, Bw, Kened Nyoni, Meneja Msaidizi Masomo ya Muda Mfupi, Chuo cha BoT, Bi. Tulla Mwigune, Meneja Idara ya Uchumi Tawi la BoT Mbeya, Dkt. Nicholaus Kessy na Mchumi Mwandamizi, Bi. Anjelina Mhoja.

Post a Comment

0 Comments