Ticker

6/recent/ticker-posts

FEDHA ZA SENSA ZISIMAMIWE VIZURI- RC SENDIGA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga akizungumza na Waratibu wa Sensa ya Watu na Makazi wa Wilaya za Sumbawanga, Nkasi na Kalambo leo ofisini kwake amabapo ameelekeza kuwa fedha za kazi hiyo zisimamiwe kikamilifu.
Mratibu wa Sensa Mkoa wa Rukwa Bw. Adam Ramadhan (kushoto ) akiwa na Mratibu Msaidizi Bw. James Kapenulo (kulia) wakiwa kwenye kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga (hayupo pichani) leo mjini Sumbawanga kujadili hali ya maandalizi ya sensa kwenye halmashauri nne za Rukwa.

(Habari na Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa)

*********************

Na.OMM Rukwa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga ametoa agizo kwa wakurugenzi wa Halmashauri za Rukwa kusimamia kwa karibu matumizi ya fedha za zoezi la Sensa ikiwemo kuhakikisha makarani wanaoendelea na mafunzo wanalipwa kwa wakati.

Ametoa agizo hilo leo (12.08.2022) alipokutana na Waratibu wa Sensa ya Watu na Makazi toka katika halmashauri za Sumbawanga, Manispaa, Kalambo na Nkasi kikao kilichofanyika ofisini kwake.

" Fedha zitoke kuanzia leo ili wakarani na wengine wanaoendelea na mafunzo walipwe. Halmashauri nitakayosikia kuna malalamiko nitachukua hatua kwa mhusika " alisema Sendiga.

Katika kikao hicho Mkuu huyo wa Mkoa alisisitiza kuwa serikali ya awamu ya sita imejipanga kuona zoezi la sensa linafanikiwa na kuwa watu wote wanahesabiwa ambapo pia amemwelekeza Katibu Tawala Mkoa huo kuhakikisha vyombo vya usafiri ikiwemo magari na mafuta vinapatikana wakati wote wa zoezi hili.

Sendiga amewahakikishia wana Rukwa kuwa changamoto zote zinafanyiwa kazi ili watu wote wahesabiwe siku ya tarehe 23 Agosti mwaka huu ili serikali ipate takwimu sahihi za idadi ya Watu.

Mkuu huyo wa Mkoa ameonya dhidi ya wale watakaokwamisha zoezi la Sensa kwa sababu zozote ikiwemo imani za dini kuwa Sheria itachukua mkondo wake kwani viashiria vimeanza kujitokeza katika baadhi ya maeneo ya Wilaya za Kalambo na Nkasi.

Kwa upande wake Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi mkoa wa Rukwa Adam Ramadhan alisema mafunzo kwa makarani, wasimamizi wa maudhui na wasimamizi wa TEHAMA yanaendelea kwenye vituo 17 kote katika halmashauri zote nne .

Adam aliongeza kusema makarani wote watapewa mikataba maalum pamoja na kula kiapo cha uadilifu ili wasimamie zoezi la sense ya watu na makazi kwa mujibu wa miongozo ya serikali iliyowekwa.

Mratibu huo alisema pia vifaa muhimu ikiwemo vishikwambi 4,220 vimekwisha gawiwa kwa washiriki wa mafunzo vikitumika kufanya maandalizi ya zoezi hilo la sensa.

Post a Comment

0 Comments