Ticker

6/recent/ticker-posts

KIWANDA CHA CHAI MPONDE KUZINDULIWA, PIA CHONGOLO ATOA ONYO KWA WAZAZI, WATOTO WA KIKE WAENDE SHULE



****************

Na Hamida Kamchalla, LUSHOTO.

KILIO cha muda mrefu cha wakulima wa zao la chai kuhusu kufufuliwa kwa Kiwanda cha Chai cha Mponde, kilichopo katika halmashauri ya Bumbuli, Wilaya ya Lushoto kimesikika ambapo kitaanza majaribio mwezi Septemba, mwaka huu baada ya serikali kuingikia kati.

Mkuu aliyasema hayo jana mbele ya Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (Ccm) Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba baada ya kuwasili wilayani Lushoto mkoani humo kuanza ziara ya siku tatu kukagua utekelezaji wa ilani ya chama hicho kupitia miradi ya maendeleo, kukagua uhai wa chama na kuhamasisha wananchi kwenye Sensa ya Watu na Makazi itakayofanywa Agosti 23, mwaka huu.

Akiwa Bumbuli, Chongolo alipokea kilio cha wananchi wa Lushoto kuhusu kiwanda hicho na ndipo mkuu wa Mkoa akatoa taarifa akisema serikali inatambua kilio hicho na imeshachukua hatua na kuwa mwezi ujao kiwanda hicho kitaanza majaribio ya kuchakata chai kwa miezi mitatu.

"Hatua zimeshachukuliwa na serikali kukifufua na mwezi ujao (Septemba majaribio ya kuchakata chai yanaanza kwa miezi mitatu na Desemba kitafunguliwa," alisema Mgumba.

Aidha akiwa katika halmashauri hiyo Chongolo alipiga marufuku watoto wa kike kuachishwa au kutopelekwa shule kwani na wao wana haki ya msingi ya kupata elimu kama watoto wa kiume.

Akiwa katika eneo la Kwehangala panapojengwa hospitali ya halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto ambayo imeanza kufikia kukamilika amefafanuavkuwa kuna baadhi ya wazazi au walezi wana tabia ya kuwakosesha watoto kwenda shule.

Chongolo amebainisha kwamba serikali imepanga kutoa elimu watoto elimu bila malipo kwa lengo la kila mtoto anayestahili kwenda shule aende kwa lengo kupata elimu.

"Ndugu zangu, mtu yeyote atakayemzuia mtoto anayestahili kwenda shule, awe wa kike au wa kiume ni marufuku, mtoto wa kike ana haki ya kupata elimu kama wa kiume, na kwenye huu Mkoa imedhihirika watoto hao wakipelekwa shule wanafanya vizuri tena wanakula bora kwelikweli, kwahiyo tusiwanyime fursa hiyo" amesema Chongolo.

"Kumuozesha binti kabla hajafikia malengo yake ni kumkatili, ni kumnyima fursa ya maisha anayostahili ambayo Mungu alimpangia, waacheni wapate elimu, siku hizi vijana wote wanataka wanawake wasomu ili wasaidiane mambo kistaarabu,

"Sasa mkimkwamisha aolewe aachike ili abaki na mateso kwasababu na yeye atakuwa hana fursa ya kujikwamua pale alipo, tengenezeni mfumo wa watoto wa kike kwenda shule, wazee wangu wangu nawaomba, ukitaka mahari nzuri ni kwa binti aliyeandaliwa vizuri, ukitaka mahari mapema binti hawezi kuwa msaada tena kwako binti ataenda kule kupitia mwanaume" amesema.

Chongolo amesema wazazi waimarishçe mazingira ya elimu ili itokee siku Ccm Katibu mkuu awe mwanamke kwakuwa tangu kuundwa kwa chama hicho haijawahi kutokea mwanamke kushika wadhifa huo

Post a Comment

0 Comments