Ticker

6/recent/ticker-posts

MRADI MKUBWA WA MAJI WA B. 40, KUANZA MWISHO WA MWAKA HUU.


Katibu mkuu wa CCM, Daniel Chongolo akimsikiliza kero za wananchi wa kata ya Mkinga alipokwenda kutembelea Shina namba 3 la Ccm katika kijiji cha Magaoni.
Mbunge wa jimbo la Mkinga Dastan Kitandula akiongea kuhusu kero ya maji mbele ya Katibu Chongolo.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali mstaafu Ngemela Lubinga akiongea na wananchi wa kata ya Mkinga

****************

Na Hamida Kamchalla, MKINGA.

SERIKALI imetenga kiasi cha sh bilioni 40 zitakazotekeleza mradi mkubwa WA maji kutoka mto Zigi jijini Tanga kupitia barabara kubwa ya Horohoro, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.

Hayo yamebainishwa jana na Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Daniel Chongolo akiwa kwenye ziara yake wilayani humo na kuongea na wananchi wa kata ya Mkinga baada ya kupokea malalamiko kuhusu kero sugu ya maji iliyopo katika Wilaya hiyo.

"Hapa mmeniambia shida ya maji, niwahakikishie, suala hili la mradi mkubwa wa maji kutoka mto Zigi kwenda Horohoro siyo hadithi kabisa, mimi Katibu mkuu wa CCM niwahakikishie tunakwenda kutekeleza, na serikali yenu imetenga sh. bilioni 40 kwa ajili ya kutekeleza mradi huu" amesema.

Aidha Chongolo amebainsha kwamba atahakikisha anasimamia utekelezaji wa mradi huo na mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu uwe umeanza kutekelezwa ili isichukue muda mrefu wananchi waondokane na kero hiyo sugu ya muda mrefu.

Chongolo akisisitiza kuwa serikali Iko kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo, hivyo haiwezi kuongea bila vitendo na inapoahodi kutekeleza ilani ya uchaguzi kwa kugusa kila idara na kwa wakati wake uliopangwa kiutekelezaji.

Naye Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Nishati na Madini Dastan Kitandula amesema shida kubwa iliyoko katika ukanda huo ni maji na kimekuea kilio kikubwa cha miaka mingi kwa wananchi wa jimbo lake.

"Watu wa Mkinga hususani wa ukanda huu wa Pwani, shida yetu kubwa ni maji hili ni tatizo kubwa, lakini tangu ameingia Muheshimiwa Rais ameingia tumekuwa na matumaini makubwa, tunakwenda kujengewa mradi mkubwa wa maji ambapo mradi huu utakapokwenda kukamilika utanufaisha watu wote wa Mkinga" amesema.

"Taarifa zilizopo ni kwamba Mkandarasi wa mradi huu ameshapatikana na kwamba wiki ya mwisho wa mwezi huu wa nane, kutakuwa na makubaliano ya uwekaji sahihi kati ya serikali na Mkandarasi ili kazi iweze kuanza" amefafanua Kitandula.

Kwa upande wake Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali mstaafu Ngemela Lubinga, alisema mabadiliko yanayoonekana ni matokeo ya utekelezaji wa ilani hivyo aliwaomba wananchi hao kutoa ushirikiano kwa serikali ili kuweza kufanikisha ilani ya CCM.

"Mabadiliko haya hayatakwenda kama hatukuyapeleka inavyotakiwa, hivyo tusimamie wote ili ilani yetu iweze kutekelezwa kama ilivyopangwa, dhamana mliyonayo ni kubwa, wananchi niwaombe niwaombe" amesisitiza Lubinga.

Post a Comment

0 Comments