Ticker

6/recent/ticker-posts

RC MGUMBA ABAINISHA VIPAUMBELE VYAKE MKOA WA TANGA, AWEKA MSISITIZO KWA ASILIMIA 40 YA MIRADI.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akiongea na watumishi wa halmashauri ya mji wa Handeni, wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala Wilaya Handeni Mashaka Mgeta.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Siriel Mchembe akisoma taarifa ya Wilaya hiyo mbele ya Waziri Masauni.
Watumishi wa halmashauri hiyo wakisikiliza mkuu wa Mkoa Mgumba akizungumxa nao.

************************

Na Hamida Kamchalla, HANDENI.


MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amewashukia watendaji katika halmashauri ya mji wa Handeni akitaka fedha za miradi ya maendeleo asilimia 40 kutumia ipasavyo lakini pia kumalizika kwa wakati kwa miradi hiyo.


Akiongea na watumishi hao katika ukumbi wa jengo la halmashauri hiyo, Mgumba amebainisha baadhi ya vipaumbele vyake katika Mkoa wa Tanga na kusema hiyo ni mojawapo katika kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi (Ccm).


Amesisitiza kwamba mtendaji yeyote atakayebainika kuchelewesha mradi atawajibika kwakuwa anafanya matumizi mabaya ya fedha kwani mradi unapozidi muda wake bila kukamilika kunatumika fedha zaidi ya zilizotengwa.


Mgumba amesema kila halmashauri ni lazima kukusanya asilimia 10 ya vijana na asilimia 40 ya miradi ya maendeleo bila kuleta visingizio vya ukusanyaji mdogo wa mapato lakini pia kubadilisha matumizi ya fedha hizo.


"Nahitaji asilimia 10 ya vijana iende, umekusanya sh milioni 1 nahitaji asilimia 40 ya maendeleo iende, sitaku kusikia makusanyo ya mapato madogo, na fedha za maendeleo zimefawanywa posho na kutumika kwenye OC hatutaelewana mkuu wa Wilaya na viongozi wengine",


"Kama unataka upate OC kubwa, kaongeze mapato, ndiyo maana serikali imeleta muongozo, halmashauri zote zenye mapato chini ya sh bilioni 5 ni lazima watenge asilimia 40 ziende kwenye miradi ya maendeleo kutatua matatizo ya wananchi na asilimia 60 matumizi ya kawaida, jipangieni mnavtoweza" amefafanua.


Aidha Mgumba amesisitiza kuwa kutokana na kiapo chake hatoweza kumkubali Wala kumvumilia yeyote katika halmashauri atakayetumia mwanya wa kisingizio cha uhaba wa mapato kwasababu atakuwa anakiuka maelekezo ya Rais, serikali pamoja na bunge.


Sambamba na hilo amesisitiza suala la kusimamia matumizi ya mapato ya ndani ya halmashauri na kuona kama fedha zilizotumika zimeweza kuondoka shida za wananchi katika halmashauri husika na siyo kwa matumizi mengine ya watumishi.


"Katika kusimamia matumizi kwa ajili ya manufaa ya wananchi, maana yake ni kwamba, tumesanya sawa, lakini je zimetumikaje, zimeweza kusaidia kuondoka shida za watu wa Handeni au zimeishia kwenye posho, nauli na mafuta, sitaku kusikia kwamba kuna halmashauri ina mapato kidogo, lugha hiyo iwe mwanzo na mwisho",


"Kwasababu kigezo cha kwanza kuanzisha halmashauri, ni kwamba ijiridhishe na iithibitishie serikali kwamba ina uwezo wa kujiendesha, haiwezi kupewa halmashauri wakati ikiwa haiwezi kujiendesha, kwahiyo suala la kuwa na mapato kidogo hiyo ni hadithi na halipo" amesisitiza Mgumba.


Hata hivyo amesema suala la usalama ni kipaumbele kingine ambacho kinabeba raia na mali zao, mipaka pamoja na chakula kwa maana ya kujihakikishia wananchi wanakuja na chakula cha kutosha na ziada ya kuuza nje kwa ajili ya kipato chao, lakini pia usalama wa uhifadhi wa misitu na mazingira pamoja na uoto wa asili.


"Kwasababu, kutokana na mabadiliko ya tabianchi, misitu iliharibika tutakwenda kukosa mvua, wananchi watalima watakoda chakula, na mtu mwenye njaa hatawaliki, sababu ataona hakuna tofauti ya kufa na kuishi, ndiomaana suala la mazingira ni suala la usalama" amebainisha.

Post a Comment

0 Comments