Ticker

6/recent/ticker-posts

WAFANYABIASHARA WASHIRIKI SENSA, RC MGUMBA ATAKA WANAFUNZI WAWEPO NYUMBANI WIKI NZIMA YA KUHESABIWA.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba katika harakati za kuhimiza sensa ya watu na makazi 2022
Wafanyabiashara wa soko la Mgandini wakiwa katika harakati za utafutaji huku wakielezea kuhusu sensa.
Mwandishi wa habari wanandamizi wa gazeti la Mwananchi mkoani Tanga, Susan Ujinga akitoa elimu ya sensa kwa wanaybiashara gulioni hapo
Mfanyabiashara wa nguo na viatu katika gulio la Tangamano, jijini Tanga.


*****************************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

WAFANYABIASHARA jijini Tanga wamesema wameiomba serikali kuiweka utaratibu wa kutoa elimu kwa shuhuli zote za Kitaifa zinazohitaji ushirikiano kutoka kwa wananchi.

Wamesema baadhi ya wananchi wamejiandaa na leo wameanza kuhesabiwa lakini hawakuwa na uelewa mpana wa maana ya sensa na kwamba wameweza kuelimishana wenyewe wanapokutana katika maeneo yao wanavyofanya biashara zao.

Baadhi yao wamefafanua kwamba leo wameshindwa kubaki nyumbani kutokana na hali ya utafutaji lakini wameacha maelezo yao kuhusu madeali ya sensa nyumbani kwao ili kutoa ushirikiano mzuri kwa makarani wanaoendesha sensa.

"Lengo la sensa limeeleweka na watu walishajiandaa kutoa ushirikiano mzuri kwa makarani wetu ili kutimiza lengo la serikali la kupata takwimu sahihi za wananchi wake, mwanzoni baadhi ya watu walikuwa hawaelewi sensa ni kitu gani wala ina maana gani, kama Mimi ninayemjua na wengine tulikuwa tunaelewesha wenzetu, kadri siku zilivyokwenda walianza kuelewa".

"Nitoe ombi kwa serikali, inapotokea linakuja swala la Kitaifa kama hii sensa, basi itoe elimu kwa shuhuli wananchi kiufasaha ili waweze kupata uelewa mapema kwani kwa kufanya hivyo elimu itasambaa kwa haraka na hakutakuwa na usumbufu wa aina yoyote" amesema Makame Bakari, anayeza bidhaa ya nazi katika soko la Mgandini.

Awali katika uzinduzi wa sensa, mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amewataka wanaomiliki shule binafsi kuheshimu shuhuli za Kitaifa kwa kufuata maelekezo ya serikali kwani katika zoezi hilo kwa wanafunzi Kuna wiki nzima ya mwisho kuanzia leo Agosti 23 pindi wanapoanza kuhesabiwa.

"Zoezi hili ni la wiki nzima kuanzia leo, lakini ajabu ni kwamba wenzetu wa shule binafsi wametoa siku mbili tu kwa wanafunzi wao kurejea shuleni mara tu baada ya kuhesabiwa, shuhuli hii ni ya Kitaifa hivyo serikali ni lazima iheshimiwe"

"Nitoe wito kwa wakuu wote wanaomiliki shule hizi hapa Mkoa wa Tanga, tunata kuona wanafuata maelekezo ya serikali na badala ya watoto kurudi shule siku mbili baada ya kuhesabiwa, sasa waongeze siku, tunaanza kuhesabiana leo hadi Agosti 29 ambapo tutahesabu watu na siku tatu za mwisho tutakuwa na sensa ya makazi" amefafanua Mgumba.

Post a Comment

0 Comments