Ticker

6/recent/ticker-posts

WANACHAMA WA NHIF WATAKIWA KUWA MABALOZI WAZURI KWA KUTOA TAARIFA SAHIHI ZA MFUKO HUO


Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) Benard Konga akizungumza kwenye kikwo cha Majadiliano ya kuboresha Mfuko huo.
Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Mwanza Jarlath Mushashu akitoa mada mbalimbali juu ya uboreshaji wa bima ya afya.
Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke akichangia mada kwenye kikao hicho
Baadhi ya wadau wa Mfuko wa Bima ya Afya wakimsikiliza kwa makini mada zinazotolewa na viongozi mbalimbali na Mfuko huo.

****************

Na SHEILA KATIKULA, MWANZA. 

Wanachama wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini (NHIF) wametakiwa kuwa mabalozi wazuri wa kutoa taarifa sahihi ili ziweze kusaidia kuepuka udanganyifu naofanywa na baadhi ya watumiaji wa mfuko huo.

Hayo amesemwa jana na Mkurugenzi wa Bima ya Afya Nchini Dk, Benard Konga kwenye kikao Cha kujadili na kupata maoni ya maboresho ya uendeshaji wa Mfuko huo.

Dk Konga amesema taarifa sahihi zitasaidia kupunguza udanganyifu ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya wanachama ambao siyo waaminifu wanaojaribu kubadirisha nyaraka za serikali.

"Tunawaomba waajili mnapokuwa mnasaini fomu za kuomba vitambulisho mjilidhishe kama hao ndiyo watengemezi halali wa mwanachama husika,"amesema Dk Konga.

Hata hivyo amesema miaka 14 hadi 15 iliyopita kulikuwa na wagonjwa wa figo 234 ambapo hivi sasa kuna wagonjwa wa figo 2000.

"Leo hii tukizungumzia miaka 15 iliyopita mfuko wa bima ya Afya ya taifa ulikuwa unatumia gharama kubwa kwenye ugonjwa wa malaria na magonjwa ya kuambukiza yanayoingia na kutoka lakini hivi sasa tunazungumzia saratani,Figo ndiyo magonjwa ambayo yanakuwa kwa kiasia kikubwa,"amesema Konga. 

Naye Mwenyekiti wa NHIF Dk, Ally Muhimbi ameshauri kuwa kuna sababu ya kupitia upya baadhi ya kanuni ili kuweza kufanyia kazi maboresho ili yaweze kuendana na wakati na mazingira ya hivi sasa.

Kwa upande wake Meneja wa Mfuko wa Bima ya afya Mkoa wa Mwanza (NHIF) Jarlath Mushashu amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya kupanda kwa gharama kumekuwa na wimbi la udanganyifu kwa baadhi ya wanachama wa Mfuko huo hali ambayo inatishia kuhujumu mfuko huo.

Naye mmoja wa washiriki wa kikao hicho Sheikh wa Mkoa Mwanza ,Hassan Kabeke ameuomba mfuko huo kushirikiana kikamilifu na viongozi wa dini zote kwa kutoa elimu ya kujiunga na mfuko huo.

Post a Comment

0 Comments