Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MULAMULA APOKEA BARUA ZA UTAMBULISHO MKURUGENZI MKAZI UNAIDS


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea Barua za Utambulisho za Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Ukimwi (UNAIDS), Bw. Martin Odiit katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

**************************

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb.) amepokea Barua za Utambulisho za Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Ukimwi (UNAIDS), Bw. Martin Odiit katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Waziri baada ya kupokea barua za utambulisho za kiongozi huyo, alipongeza jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na shirika hilo hasa kutoa elimu na kampeni dhidi ya Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ambapo kupitia kampeni hizo zimesaidia maambukizi ya ugonjwa huo kupungua.

Balozi Mulamula amemhakikishia ushirikiano wa kutosha kutoka Serikalini wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake hapa nchini na kuongeza kuwa UNAIDS imesaidia kupunguza maambukizi ya UKIMWI kwenye jamii.

Nae, Mkurugenzi Mkazi wa UNAIDS, Bw. Martin Odiit amesema kuwa shirika hilo litaendselea kuelimisha jamii ya kitanzania na kuhakikisha kuwa kufikia mwaka 2025 Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto atakayezaliwa yatakuwa yamepungua kwa asilimia 95.

“Tupo hapa ili kuhakikisha kuwa tunashirikiana na Serikali kutoa elimu kwa jamii ili kuweza kuwa na uelewa utakao saidia kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi,” amesema Bw. Odiit

Post a Comment

0 Comments