Ticker

6/recent/ticker-posts

RC MJEMA AZINDUA VITABU VYA KUBORESHA USIMAMIZI WA ELIMU

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akionesha Vitabu vya Kuboresha Usimamizi wa Elimu.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema amezindua Vitabu vya Kuboresha Usimamizi wa Elimu kwa mkoa wa Shinyanga ambavyo ni pamoja na kitabu cha Mkakati wa Kuimarishaji Ufundishaji na Ujifunzaji Ngazi ya Elimu Msingi, Kitabu cha Changamoto katika Uboreshaji wa Elimu Msingi na Sekondari. Nini Kifanyike? pamoja na Kitabu cha Mwongozo wa Uteuzi wa Viongozi wa Elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mikoa.

Uzinduzi wa Vitabu vya Kuboresha Usimamizi wa Elimu kwa mkoa wa Shinyanga umefanyika leo Jumanne Septemba 6,2022 katika Ukumbi wa Chuo Cha Ualimu Shinyanga (SHY COM) Mjini Shinyanga baada ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kufanya Uzinduzi wa Vitabu hivyo kitaifa Agosti 4,2022 mkoani Tabora.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema amesema vitabu hivyo vitasaidia kuboresha usimamizi wa elimu mkoani Shinyanga huku akisisitiza kuwa anataka kuona mabadiliko mkoani Shinyanga na kuhakikisha walimu na wanafunzi wanalindwa na watoto wanasoma na kufaulu na walimu wanakuwa na nidhamu.

“Ili kuboresha elimu tuna wajibu kufanya kazi kwa kujituma na kushirikiana. Tuhakikishe tunadhibiti utoro, tuhakikishe kuwa watoto hawaolewi wangali wadogo,kusiwe na mimba za utotoni, watoto wafuatiliwe waende shule na Watoto wadogo chini ya miaka 18 wasiwe wafanyakazi wa ndani bali wapelekwe shule na wazazi tuhakikishe tunalinda watoto huku tushirikiana na walimu. Pia kuwe na mikakati ya kuwashirikisha wazazi kushiriki maendeleo ya shule”,amesema Mjema.

Mkuu huyo wa mkoa huo ametumia fursa hiyo kuwakumbusha na kuwatadharisha wazazi na walezi kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watoto kwani kuna mambo mabaya mtandaoni ambayo hayapaswi kuonwa na watoto.

“Tuwafundishe watoto kuhusu TEHAMA lakini tuzuie watoto kuingia kwenye mitandao isiyofaa. Kwenye mitandao ya kujamii kuna mambo ya ajabu sana, Hakikisheni mnalinda watoto dhidi ya mitandao ya kijamii kwani mtoto anaweza kujifunza mambo mabaya ana akayafanya kwa vitendo”,amesema Mjema.

Aidha amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa walimu na kuondoa mazingira ya udhalilishaji kwa walimu huku akiwataka walimu kujiheshimu na kulinda heshima ya ualimu.

“Tutaendelea kuboresha miundombinu ya shule pamoja na kuondoa mazingira ya udhalilishaji kwa walimu. Lakini na nyinyi walimu jiheshimuni, mkijiheshimu jamii itawaheshimisha, msivae mavae ya ajabu ajabu na mjitahidi kuwa na lugha nzuri. Jiwekeni kwenye hali ambayo mtaweza kujiheshimu”,amesema Mjema.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akizindua Vitabu vya Kuboresha Usimamizi wa Elimu kwa mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Septemba 6,2022 katika ukumbi wa Chuo cha SHYCOM Mjini Shinyanga. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo, kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akionesha Vitabu vya Kuboresha Usimamizi wa Elimu ambavyo ni pamoja na kitabu cha Mkakati wa Kuimarishaji Ufundishaji na Ujifunzaji Ngazi ya Elimu Msingi, Kitabu cha Changamoto katika Uboreshaji wa Elimu Msingi na Sekondari. Nini Kifanyike? pamoja na Kitabu cha Mwongozo wa Uteuzi wa Viongozi wa Elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mikoa. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo, kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akionesha Vitabu vya Kuboresha Usimamizi wa Elimu ambavyo ni pamoja na kitabu cha Mkakati wa Kuimarishaji Ufundishaji na Ujifunzaji Ngazi ya Elimu Msingi, Kitabu cha Changamoto katika Uboreshaji wa Elimu Msingi na Sekondari. Nini Kifanyike? pamoja na Kitabu cha Mwongozo wa Uteuzi wa Viongozi wa Elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mikoa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akionesha Vitabu vya Kuboresha Usimamizi wa Elimu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akikabidhi Vitabu vya Kuboresha Usimamizi wa Elimu kwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo kwa ajili ya kuvikabidhi kwa viongozi wa ngazi ya wilaya.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akizungumza wakati akizindua Vitabu vya Kuboresha Usimamizi wa Elimu kwa mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Septemba 6,2022.

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof, Siza Tumbo na Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako (kulia) wakisikiliza hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akizindua Vitabu vya Kuboresha Usimamizi wa Elimu kwa mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Septemba 6,2022.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akizindua Vitabu vya Kuboresha Usimamizi wa Elimu kwa mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Septemba 6,2022.

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof, Siza Tumbo akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akizindua Vitabu vya Kuboresha Usimamizi wa Elimu kwa mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Septemba 6,2022.
Mstahiki Meya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akizindua Vitabu vya Kuboresha Usimamizi wa Elimu kwa mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Septemba 6,2022.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema (kushoto) akiteta jambo na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof, Siza Tumbo wakati wa uzinduzi wa Vitabu vya Kuboresha Usimamizi wa Elimu kwa mkoa wa Shinyanga
Wadau wa elimu wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa Vitabu vya Kuboresha Usimamizi wa Elimu

Wadau wa elimu wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa Vitabu vya Kuboresha Usimamizi wa Elimu.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Post a Comment

0 Comments