Ticker

6/recent/ticker-posts

BEI ZA BIDHAA ZA MAFUTA NCHINI ZASHUKA KWA MWEZI SEPTEMBA 2022

*Serikali yatoa ruzuku tena ya bilioni 65 kwa mafuta ya Dizeli kutokana na mahitaji yake makubwa

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za
bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini ambapo bei hizo zimeanza kutumika kuanzia Septemba 7, 2022 lengo ni kutaka wananchi wapate huduma bora bila ya kuwepo ongezeko la litalofanya wananchi waumie katika kupata nishati hiyo .

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi Modestus Lumato ilisema bidhaa za mafuta ya mafuta katika soko la dunia za Julai 2022 zimepungua ikilinganishwa na bei hizo
kwa Juni 2022.

Hivyo, bei za mafuta katika soko la ndani zimepungua vilevile kwa kati ya shilingi 271/lita na shilingi 362/lita kwa petroli na kwa shilingi 430/lita kwa mafuta ya taa ukilinganisha na bei zenye ruzuku za Agosti 2022.

Kwa mafuta ya dizeli, ukiiacha bei ya Tanga ambayo inashuka kwa shilingi 13/lita, bei za Septemba 2022 zimeongezeka kwa
shilingi 37/lita na shilingi 86/lita kwa Dar es Salaam na Mtwara, sawia, ukilinganisha na bei zenye ruzuku za Agosti 2022 ili kuendelea kupunguza madhara ya ongezeko la bei za dizeli hapa nchini ambapo shughuli nyingi za kiuchumi zinategemea dizeli na pia ili
kupunguza tofauti kati ya bei za petroli na dizeli, Serikali imetoa ruzuku ya shilingi bilioni 65 ili kupunguza bei za mafuta za mwezi Septemba 2022. Kwa kutoa ruzuku hiyo,

Serikali imepunguza bei za bidhaa za mafuta kwa mwezi Septemba 2022 kwa Dar es Salaam bei i za Mafuta kwa mwezi Septemba 2022 kabla na baada ya ruzuku Petroli shilingi 3049 baada ya ruzuku shilinh 2969 na Dizeli shilingi
shilingi/lita 3359 baada ya ruzuku shilingi 3125.

Mhandisi Lumato katika taarifa hiyo inafafanunua kuwa Mafuta katika soko la dunia zimepungua ikilinganishwa na bei za mwezi Juni 2022 na kufanya kwa bei za mafuta katika soko la ndani zimepungua kati ya shilingi 271 kwa lita na shilingi 362 kwa lita kufikia kusababisha bei za mafuta katika soko la ndani kuongezeka pia na ili kupunguza madhara ya ongezeko hilo katika soko la ndani.

Amesema kuwa Serikali kwa kutoa ruzuku hiyo imepunguza bei za bidhaa za mafuta kwa Septemba 2022 ambapo bei hizo zinatofautiana kutokana na umbali kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kadri ya umbali unapokuwa mrefu ruzuku yake inakuwa kubwa.

Bei za mafuta kabla ya ruzuku, Agosti 2022 baada ya ruzuku pamoja na Kiwango cha Ruzuku kwa Petroli kwa mkoa wa Dar es Salaam bei petroli 3636 baada ya ruzuku 3410 kiwango cha ruzuku 220 hivyo mfano huo kwa Mkoa huo inaonyesha sehemu nyingine beo zinapanda kutokana na umbali.

Kwa taarifa hiyo ilibainisha kuwa katika kutekeleza bei hizo wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta watatakiwa kuzingatia kwa EWURA kuukumbusha umma kwamba bei kikomo za bidhaa za

Mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana pia kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo.

Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.

Amesema kuwa Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko na EWURA hiyo itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.

Taarifa hiyo ilisema bei zinazotolewa lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta na Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi tu bei hizo zisivuke bei kikomo au kushuka chini ya bei iliyoruhusiwa kama ilivyokokotolewa kwa kutumia fomula na Kanuni za EWURA za kupanga bei za Mafuta za mwaka 2022 zilizotangazwa.

Aidha katika taarifa hiyo ya Mkuruguenzi Mkuu Mhandisi Lumato inasema vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani.

Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja.

Aidha amesema adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika na Wauzaji wa mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa risiti za mauzo kutoka kwenye Mashine za EFPP na Wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita.

Stakabadhi hizo za malipo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya aidha kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora kinachofaa na pia, risiti hizo zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mauzo ya mafuta ya petroli.

Hata hivyo taarifa hiyo ilidokeza kuwa Wauzaji wa Mafuta ya petroli wa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei yenye ruzuku na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiu agizo hilo
mafuta kwa bei yenye ruzuku.

Post a Comment

0 Comments