Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DKT.HUSSEIN MWINYI AFUNGUA MASJID HUDA MASINGINI KMKM NA KUJUMUIKA KATIKA SALA YA IJUMAA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria kufungua Masjid Huda ulioko Masingini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja leo 23-9-2022,kabla ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid hiyo (kulia kwa Rais) Mkurugenzi Mkuu wa Al Noor Charitable Agency Zanzibar.Sheikh Nadir Mahfoudh na Sheikh Luay Mohammed Mahfoudh na (kushoto kwa Rais) Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Alhaj Haroun Ali Suleiman.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akifuatilia Hutuba ya Sala ya Ijumaa ikisomwa na Sheikh Abdulkarim Said, iliyofanyika katika Masjid Huda Masingini baada ya kuufungua Msikiti huo leo 23-9-2022 na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Alhaj Haroun Ali Suleiman.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Waumini wa Dini ya Kiislam Masingini Wilaya ya Magharibi “A”Unguja, baada ya kuufungua Msikiti huo na Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Huda leo 23-9-2022.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Ufunguo wa Masjid Huda Imamu Mkuu wa Msikiti huo Sheikh Ali Rashid Khamis, baada ya kumalizika Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti huo uliofunguliwa leo 23-9-2022.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments