Ticker

6/recent/ticker-posts

TBS YATOA MAFUNZO KWA WADAU WA ZAO LA MUHOGO MKOA WA LINDI NA MTWARA


Meneja wa Utafiti na Mafunzo Bw.Hamis Sudi Mwanasala akizungumza na washiriki wa mafunzo kwa wajasiriamali ambao ni wazalishaji, wasindikaji, wakulima na wauzaji wa bidhaa za muhogo kutoka wilayani Newala mkoani Mtwara. 

Washiriki wa mafunzo kwa wajasiriamali ambao ni wazalishaji, wasindikaji na wauzaji wa bidhaa za muhogo wilayani Masasi mkoani Mtwara. 

Washiriki wa mafunzo kwa wajasiriamali ambao ni wazalishaji, wasindikaji na wauzaji wa bidhaa za muhogo wilayani Nachingwea mkoani Lindi. 

Meneja wa Kanda ya Kusini Bi. Amina Yassin akizungumza na washiriki wa mafunzo kwa wajasiriamali ambao ni wazalishaji,wasindikaji na wauzaji wa bidhaa za muhogo kutoka wilayani Masasi. 

Washiriki wa mafunzo kwa wajasiriamali ambao ni wazalishaji,wasindikaji na wauzaji wa bidhaa za muhogo kutoka wilayani Mtama mkoani Lindi. 

*************** 

Na Mwandishi Wetu 

WAJASIRIAMALI ambao ni wazalishaji, wasindikaji na wauzaji wa bidhaa za muhogo katika wilaya nne za Nachingwea, Masasi, Mtama na Newala katika Mikoa ya Lindi na Mtwara wametakiwa kuzalisha bidhaa hizo kwa kuzingatia viwango ili kuziwezesha kushindana katika masoko ya ndani, kikanda na kimataifa. 

"Mkijibidisha na kuzalisha muhogo wa kutosha na kusindika muhogo wenye ubora, mtaweza kufanikisha adhima ya Serikali ya kuendeleza viwanda na kutoa ajira kwa kada mbalimbali pamoja na kuwezesha bidhaa kushindana." 

Wito huo ulitolewa kwa nyakati tofauti na Meneja wa Utafiti na Mafunzo wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Hamisi Sudi, wakati akieleza washiriki wa mafunzo umuhimu wa mafunzo hayo kwa washiriki hao wa wilaya hizo nne. 

Sudi aliwataka wajasiriamali hao kujibidisha na kuzalisha muhogo wa kutosha kwa kuzingatia viwango, ubora na usalama ili kulinda afya ya mlaji na kujenga uchumi wa Taifa kwa ujumla. 

"Pia huu ni uthibitisho wa nia ya Serikali kupitia taasisi zake katika kufanikisha malengo ya Taifa letu ya ujenzi wa uchumi kupitia uwekezaji katika viwanda,"alisema Sudi. 

Kwa upande wake Meneja wa TBS Kanda ya Kusini, Amina Yassin, aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kutambua kwamba azma ya Serikali ni kukuza viwanda ili Taifa liweze kujitosheleza kwenye uzalishaji wa bidhaa mbalimbali. 

"Hivyo tukijibidisha kuzalisha muhogo wa kutosha na kusindika muhogo wenye ubora tutaweza kufanikisha adhima hii," alisema Yassin na kuongeza; 

"Hivyo nawasihi tuendelee kuzalisha muhogo na bidhaa za muhogo kwa kuzingatia viwango." Miongoni mwa mada zilizotolewa kwenye mafunzo hayo ni viwango na faida zake, matakwa ya kiwango cha muhogo, kanuni bora za kilimo cha muhogo, kanuni bora za usindikaji, kanuni bora za afya na teknolojia za usindikaji wa bidhaa za muhogo. 

Nyingine ni vifungashio na ufungashaji wa bidhaa muhogo na bidhaa za muhogo, huduma kutoka dawati la Ofisi ya Maendeleo ya Jamii, usajili wa biashara, Utaratibu wa udhibitishaji ubora wa bidhaa na usajili wa majengo na bidhaa za chakula. 

Mada hizo zilitolewa na maofisa wa TBS, SIDO na TAMISEMI. Baada ya mafunzo hayo kulikuwa na fursa kwa washiriki waliokuwa tayaru kutembelewa ili kupewa mafunzo zaidi na ushauri katika maeneo yao ya usindikaji. 

Mafunzo hayo yaliwalenga wajasiriamali ambao ni wazalishaji, wasindikaji na wauzaji wa bidhaa za muhogo ambao tayari ziko kwenye soko, lakini hazijathibitishwa na TBS katika wilaya hizo nne.

Post a Comment

0 Comments