Ticker

6/recent/ticker-posts

TEA YAKABIDHI  JUMLA YA TAULO ZA  KIKE BOKSI 62 KAMPENI YA MTHAMINI


Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imekabidhi taulo za kike jumla ya box 62 zenye thamani shiling 1,500,000 inayojumuisha mchango wa Taasisi na michango ya watumishi wa TEA.

Taulo hizo zimetolewa katika Kampeni maalum ijulikanayo kama ‘‘NAMTHAMINI’’ inayolenga kuchangisha taulo za kike kwa wanafunzi wenye uhitaji mashuleni ambapo kampenii hiyo inaendeshwa na uongozi wa EATV.

Akizungumza kwenye tukio lililofanyikaleo Septemba 29,2022, Mkurugenzi Mkuu TEA , Bi.Bahati I. Geuzye wameahidi kuendelea kuunga mkono kampeni hiyo wakitambua umuhimu wake na kuhamasisha Taasisi zingine na watu binafsi kujitokeza kuchangia taulo hizi za kike kwa wanafunzi wenye uhitaji mashuleni.

"Ni matumani yetu kuwa ushirikiano wetu wa karibu na EATV utaongeza na kuinua upatikanaji wa elimu bora kwa usawa nchini kote". Amesema Bi.Geuzye.

Aidha ameupongeza Uongozi wa EATV kutambua na kuona changamoto zinazowakabili watoto wa kike hasa wanaotoka katika mazingira magumu na kuwafanya washindwe kuhudhuria na kufurahia masomo wanapokuwa shuleni.

Post a Comment

0 Comments