Ticker

6/recent/ticker-posts

TMA YATOA UTABIRI WA MSIMU MVUA ZA VULI KUWA UTAKUWA NA MVUA ZA CHINI YA WASTANI HADI WASTANI.



*********************

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) katika utabiri wake wa hali ya hewa wa msimu wa mvua za Vuli 2022 kwa maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka imesema msimu wa mvua za vuli utakuwa na mvua za chini ya wastani na wastani katika maeneo mengi nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo Septemba mbili, Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Agnes Kijazi amesema Kutokana na mifumo ya hali ya hewa ilivyo kwa sasa na inavyotarajiwa katika kipindi chote cha msimu, kwa ujumla kutakuwa mvua za chini ya wastani hadi wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.

Ameongeza kuwa Msimu unatarajiwa kuanza kwa kuchelewa na kuambatana na mtawanyiko wa mvua usioridhisha, Ambapo Vipindi virefu zaidi vya ukavu vinatarajiwa katika miezi ya Oktoba na Novemba 2022.

Dkt. Kijazi aliongeza kuwa kutakuwa na vipindi vya ongezeko dogo la mvua vlinalotarajiwa kujitokeza katika maeneo machache hususani wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Disemba 2022.

"Kwa kawaida msimu wa mvua za Vuli huisha mwezi Disemba. Hata hivyo, kunatarajiwa kuwepo na muendelezo wa mvua kwa mwezi Januari, 2023”. Alisema Dkt Kijazi

Post a Comment

0 Comments