Ticker

6/recent/ticker-posts

UDSM YATOA MSAADA SHULE YA MSINGI SINZA MAALUMU

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye akikabidhi vifaa mbalimbali kwa shule ya msingi Sinza Maalumu leoSeptemba 16,2022 Jijini Dar es Salaam.Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye akizungumza katika zoezi la utoaji msaada wa vifaa mbalimbali kwa shule ya msingi Sinza Maalumu leo Septemba 16,2022.

************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KATIKA kuendelea kusheherekea miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo Septemba 16,2022 kimetoa msaada wa wa vifaa vya kujifunzia na vifaa vya michezo katika shule ya msingi Sinza Maalumu iliyopo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika zoezi hilo la utoaji msaada, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye amesema Chuo kinathamini kazi ambayo inaendelea kufanywa na walimu katikakituo hicho ndo maana wakaamua kuwaunga mkono kwa kuwapatia baadhi ya vifaa ikiwemo viti mwendo, runinga, radio, jezi za michezo, mipira, meza, viti na baadhi ya vifaa vya kujifunzia shuleni.

"Licha ya kutoa msaada huu, tumeahidi tutaendelea kushirikiana nao kuhakikisha kwamba hakuna kinachokwama katika kuhakikisha watoto wanaohitaji elimu au watoto wenye mahitaji maalumu wanafanikiwa". Amesema Prof.Anangisye

Nae Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi sinza Maalumu, Bi.Catherine Msense ameupongeza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwani vifaa hivyo vitakwenda kusaidia wanafunzi hao kuweza kujimudu na kujihudumia pamoja na kujifunza.

Amesema shule hiyo imekuwa ikiwafundisha wanafunzi ambao wanachangamoto ya ulemavu wa akili pamoja na usonji hivyo kupitia msaada huo utakwenda kupunguza changamoto ambazo wamekuwa nazo kwa muda mrefu.
Profesa Aldin Mutembei, Profesa wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere cha Kiswahili akizungumza katika zoezi la utoaji msaada wa vifaa mbalimbali kwa shule ya msingi Sinza Maalumu leo Septemba 16,2022.

Post a Comment

0 Comments