Ticker

6/recent/ticker-posts

UDSM YAWATAKA VIJANA KUYATUMIA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KUYATEKELEZA KWA VITENDO


*********************

Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Kimewataka Vijana wanaopatiwa Mafunzo ya Ujasiriamali kwenda kuyatumia na kuyatekeleza Mawazo yao ya biashara kwa Vitendo ili kuweza kukuza biashara zao na kuajiri wenzao.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa kitengo cha ujasiriamali na ubunifu kutoka UDSM, Dkt Wini Nguni wakati akizungumza kando ya Mafunzo ya awamu ya tatu ya ujasiriamali kwa wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu Tanzania kwa mwaka 2022 ambapo amesema lengo la Mafunzo hayo ni kuongezea vijana waliohitimu taarifa na uwezo wa kujiajiri na hivyo kusaidia ukuaji wa biashara ndogo na za kati.

Amesema mafunzo hayo yanalenga vijana waliohitimu ndani ya miaka mitatu iliyopita kuanzia ngazi ya stashahada na kuendelea wenye nia ya kujiajiri,na walio na mawazo ya biashara au walioanzisha na kuwa na uzoefu wa angalau mwaka mmoja katika kuendesha biashara zao.

Aidha amesema mafunzo yanatolewa katika makundi ya watu wasiozidi 50 kwa darasa ,kwa muda wa siku nne mfululizo huku washiriki hawatalipa ada yoyote lakini watajigharamikia usafiri na malazi na kutakiwa kujaza timu ya maombi mtandao kupitia https://udsm-gep.ac.tz wakiwmbatanisha majina yao,namba za simu na mkoa watakaohudhuria mafunzo hayo.

Katika hatua nyingine amesema Mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam kuanzia septemba 27hadi Oktoba 6,2022 huku kwa mikoa ya Dodoma kisini Pemba, Mjini Magharibi,Mwanza,Mbeya, Tabora na Kuvuma yataanza Oktoba 12 hadi 20, 2022.

Kwa upande wake mmoja wa wanufaika wa Mafunzo hayo kwa mwaka uliopita Monica Warioba, amewasihi vijana wanaopatiwa Mafunzo hayo kutokukata tamaa na kusimamia mawazo yao ili kuweza kufikia ndoto zao kupitia ujasiriamali.

Naye Afisa Mwandamizi mkuu wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kitengo cha Elimu na huduma kwa mlipa kodi, Amesema kuwa lengo lako kufika hapo ni kutoa elimu ya kuwasaidia kwenda kuwapa maelekeo mzuri wa kuwa walipa kodi wajao ili kuweza kuichangia katika mapato ya serikali.

Mpaka sasa UDSM imeshatoa Mafunzo kwa vijana wahitimu 2,795 kwa mwaka 2019,1600 kutoka vyuo 75 katika mikoa 10 ambayo ni Dar es salaam, Dodoma,Mwanza,Arusha,Lindi,Iringa,Katavi,MbeyaUgunja Mjini na kubaini Pemba walipatiwa Mafunzo huku Jumla ya wahitimu 1,195 wamepatiwa mafunzo hayo kwa mwaka 2021 katika mikoa 11 huku kwa mwaka 2020 mafunzo hayo hayakufanyika kwa sababu ya mlipuko wa ugonjwa wa Uviko 19.

Post a Comment

0 Comments