Ticker

6/recent/ticker-posts

VIKAO VYA UONGOZI CCM NGAZI YA TAIFA KUFANYIKA JIJINI DODOMA

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuwataarifu wanachama wake na watanzania wote kuhusu kufanyika kwa vikao vya kawaida vya uongozi ngazi ya Taifa Jijini Dodoma kuanzia tarehe 26 Septemba, 2022 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (CC) na tarehe 27 na 28 Septemba, 2022 Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa (NEC).

Pamoja na mambo mengine vikao hivi vitakuwa na kazi ya kupokea mapendekezo, kujadili, kupitisha na kufanya uteuzi wa mwisho wa wanachama ambao wameomba uongozi katika ngazi ya wilaya.

Vikao hivyo vilitanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Kilichofanyika tarehe 22 na 23 Septemba, 2022 Jijini Dodoma.

Post a Comment

0 Comments