Ticker

6/recent/ticker-posts

WATU WAWILI WAFA KATIKA AJALI YA NOAH SINGIDA, AKIWEPO KATIBU WA MSIKITI ALIYEKUWA AKIENDA KUMPOKEA MUFTI WA TANZANIA

Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Singida wakiangalia ajali ya magari mawili aina ya Noah yaliyopata ajali leo Septemba 18, 2022 eneo la Utaho wilayani Ikungi kwa kuhusisha magari namba T 433 AUY na T 835 CJX na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi wengine saba.
Muonekano wa magari hayo baada ya ajali.
Wananchi wakiangalia ajali hiyo.
Ni huzuni tupu eneo la ajali.
Vijana wakiwa eneo la ajali hiyo.
ni huzuni tupu eneo la ajali.
Askari wa usalama akiongoza magari wakati yakipita eneo la ajali.


*******************


Na Dotto Mwaibale, Singida


WATU wawili wamefariki dunia baada ya magari aina ya Noah waliokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso eneo la Utaho Barabara Kuu ya kutoka Dodoma kwenda Singida wilayani Ikungi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Stellah Mutabihirwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea leo Septemba 18, 2022 majira ya mchana katika eneo hilo.

Mutabihirwa alisema watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni wanaume akiwepo Katibu wa Msikiti wa Kati (BAKWATA) mjini hapa aliyefahamika kwa jina la Hamisi Dinya ambaye alikuwa akienda kumpokea Mufti wa Tanzania Sheikh Dk. Abubakar Zuberi Bin Ally wa Mbwana ambaye ameanza leo ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani hapa pamoja na mtoto mmoja ambaye jina lake halijafahamika.

Alisema majeruhi katika ajali hiyo ni saba na kuwa walikimbizwa Hospitali ya Misheni ya Puma kwa ajili ya matibabu na kuwa hali ya majeruhi mmoja ni mbaya.

Kamanda Mutabihirwa alisema chanzo cha ajali hiyo ni moja ya magari hayo lililokuwa likitokea Ikungi kuelekea Singida mjini dereva wake kuwa katika mwendo mkali huku akijaribu kuyapita magari mawili kwa mpigo hivyo kushindwa kulimudu na kusababisha ajali hiyo.

Post a Comment

0 Comments