Ticker

6/recent/ticker-posts

ZAIDI YA WATOTO 990 WENYE UMRI CHINI YA MIAKA MITANO KUPATIWA CHANJO YA POLIO



**************************

Na Sheila Katikula Mwanza.

Jumla ya watoto 994,109 wenye umri chini ya miaka mitano wanatarajia kupewa chanjo ya polio awamu ya tatu ya kuzuia ugonjwa wa polio.

Hayo yamesemwa jana na Mratibu wa chanjo Mkoa wa Mwanza Amos Kiteleja wakati akizungumza na Sayari news ofisini kwake.

Amesema dozi 1,040,000 za Chanjo ya polio zimepokelewa na kusambazwa katika Halmashauri zote za mkoani hapa , timu 2,308 zenye watumishi 6,924 zitashughulika kwenye zoezi hilo.

"Timu 2,308 zenye watumishi 6,924 zitashughulika kwenye zoezi hilo ikiwamo timu moja itakuwa na watumishi watatu mchangaji,mtunza takwimu na mhamasishaji kampeni hii itafanyika nyumba kwa nyumba na kwenye sehemu maalumu,"amesema kiteleja.

Kiteleja amesema Tanzania iliendesha kampeni ya Chanjo ya kuzuia ugonjwa wa polio awamu ya pili Mei 18 hadi 21 mwaka huu na Mkoa wa Mwanza ulifanya zoezi hilo kwa ufanisi ambapo jumla ya watoto 965,229 walipata Chanjo sawa na asilimia 114 kati ya watoto 846.773 waliolengwa.

Halmashauri zote zilifanikiwa kuchanja juu ya lengo lililokuwa limewekwa kampeni hiyo iliendeshwa ukiwa ni nguzo moja wapo ya kukabiliana na ugonjwa huo ambao ulitokea nchi jirani ya Malawi pamoja na Msumbiji," amesema Kiteleja.

"Ugonjwa huu ni hatari ulitokea nchi jirani na unashambulia mfumo wa hafamu na matokeo yake huleta madhara kwa watoto chini ya miaka mitano ili kuepuka virusi vya polio visiingie nchini ikabidi kuendesha kampeni hii ya chanjo inayotolewa kwa njia ya matone mdomoni kwani zoezi hilo linatarajiwa kufanyiwa kwa awamu nne na hivi sasa ni awamu ya tatu",amesema Kiteleja.

Amesema endapo mtoto asipopata chanjo hiyo ya polio anaweza kupata ugonjwa wa kupooza, ulemavu wa kudumu na wakati mwingine kupelekea kifo.

Hata hivyo amewataka wazazi na walezi kushiriki katika zoezi hilo na kuhakikisha watoto wanapewa Chanjo hiyo.

Post a Comment

0 Comments