Ticker

6/recent/ticker-posts

ASILIMIA 70 YA VIFO HUSABABISHWA NA MAGONGWA YASIYOAMBUKIZA

Mratibu wa kituo cha kuratibu matukio ya dharula ya afya ya jamii kutoka hospitali ya Mkoa ya Rufaa ya Sekou Toure, Dk Nangi Nangi akizungumza na waandishi wa habari sababu zinazopelekea kupata magonjwa yasiyoambukiza.

**********

NA SHEILA KATIKULA, MWANZA

Asalimia 70 ya vifo duniani husababishwa na magonjwa yasiyoambukiza kwa kutoushughulisha mwili kwa kufanya kazi ,mazoezi na kubweteka.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa kituo Cha kuratibu Matukio ya dharula ya afya ya jamii kutoka Hospitali ya Mkoa ya Rufaa Sekou toure Mkoani Mwanza Dk Nangi Nangi amesema kuwa magonjwa hayo yanamadhara kwani hupelekea umasikini ndani ya jamii.

Nangi amesema ni vema kuweka utaratibu wa kufanya mazoezi sanjari na kubadili mtindo wa maisha kwa kufuata kanuni za afya ili kuweza kuwa na afya bora na kuepuka na magonjwa hayo.

"Ili tuweze kuepukana na magonjwa hayo ni lazima ulaji wetu uwe mzuri na kupunguza ulaji wa sukari, mafuta, chumvi na kujishughulisha mwili Kwa kufanya mazoezi asubuhi na jioni Kwa kutembea na kukimbia Kwa kufanya hivyo mwili utachangamka na kutopata magonjwa yasiyoambukiza.

Nangi ameyataja baadhi ya magonjwa yasiyoambukiza yanayohatalisha maisha ya binadamu kuwa ni pamoja na ugonjwa wa moyo, Kansa, kisukari, saratani pamoja na tatizo la upumuaji .

Amesema tafiti zimefanyika na kubaini vyanzo vinavyoweza kusababisha magonjwa hayo ni pamoja na matumizi ya tumbaku, unywaji wa pombe kupitiliza, maisha bwete, kula vyakula vya sina moja , uvutaji siagara pamoja na utumiaji wa ugoro.

"Ukiwa mgonjwa hauna muda wa kufanya shughuli za uzalishaji na badala yake unaangaika kutafuta tiba ili uweze kurudi katika hali yako ya awali," amesema Nangi.

Ameleza kuwa matumizi ya tumbaku na uvutaji wa siagara husababisha Kansa ya mapafu, unywaji wa pombe kupindukia husababisha sumu kuongezeka mwilini pamoja na kuishi maisha bwete.

Aidha ameeleza kuwa kutokana na Tanzania kuwa mwanachama wa shirika la Afya duniani hivyo kelekea siku ya maadhimisho ya magonjwa yasiyoambukiza Kitaifa yanatarajia kufanyika Mkoani Mwanza hivi karibuni huku kauli mbiu ikiwa badili mtindo wa maisha kuwa afya bora.

Post a Comment

0 Comments