Ticker

6/recent/ticker-posts

DART NA JESHI LA POLISI TENGENEZENI MIFUMO YA UTOAJI WA TAARIFA KUONDOA MISUGUANO-DC UBUNGO

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe.Kheri James akizungumza katika kikao cha pamoja cha wadau wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka kilichowakutanisha baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi, Wakuu wa Wilaya pamoja na DART akiwa kama mwenyeji.Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James akizungumza katika kikao cha pamoja cha wadau wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka kilichowakutanisha baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi, Wakuu wa Wilaya pamoja na DART akiwa kama mwenyeji.Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Dk.Edwin Mhede akizungumza katika kikao cha pamoja cha wadau wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka kilichowakutanisha baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi, Wakuu wa Wilaya pamoja na DART akiwa kama mwenyeji. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Dk.Edwin Mhede akizungumza katika kikao cha pamoja cha wadau wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka kilichowakutanisha baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi, Wakuu wa Wilaya pamoja na DART akiwa kama mwenyeji.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni katika kikao cha pamoja cha wadau wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka kilichowakutanisha baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi, Wakuu wa Wilaya pamoja na DART akiwa kama mwenyeji.Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma Nyangasa akizungumza katika kikao cha pamoja cha wadau wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka kilichowakutanisha baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi, Wakuu wa Wilaya pamoja na DART akiwa kama mwenyeji.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Godwin Gondwe akizungumza katika kikao cha pamoja cha wadau wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka kilichowakutanisha baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi, Wakuu wa Wilaya pamoja na DART akiwa kama mwenyeji. Baadhi ya wadau mbalimbali wakifuatilia wakati wa kikao cha pamoja cha wadau wa usafiri wa kilichowakutanisha baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi, Wakuu wa Wilaya pamoja na DART akiwa kama mwenyeji.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

***********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MKUU wa Wilaya ya Ubungo Kheri James ameutaka Uongozi wa Wakala wa Mabasi yaendayo Kasi (DART) pamoja na Jeshi la Polisi kutengeza mifumo ya ndani ya taarifa itakayosaidia kuondoa misuguano wakati wa matumizi ya Barabara za Dart.

Aidha amewataka viongozi na watumishi wote wa Umma kutimiza kwa kuzingatia na kuheshimu sheria na taratibu zote za matumizi ya miundombinu ya DART na hivyo kujiepusha na mikono ya sheria kwa kuwa hakuna yeyote aliyepo juu ya Sheria.

Ametoa kauli hiyo leo Oktoba 4,2022 wakati wa kikao cha pamoja cha wadau wa usafiri wa kilichowakutanisha baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi, Wakuu wa Wilaya pamoja na DART akiwa kama mwenyeji.

" Lengo ni kuhakikisha nyotekama wadau muhimu mnakuwa kitu kimoja kusimamia kikamilifu miundombinu ya mwendokasi ili iweze kulindwa, katika kufikia hilo, ninyi kama sehemu ya Serikali mnapaswa kuwa kitu kimoja" Amesema

Aidha kuhusu magari ya Polisi kutumia Barabara hizo, James amesema kwa sasa kinachopaswa kufuatwa ni agizo la IGP Wambura, lakini DART na Polisi Wana kila sababu ya kukaa pamoja na kuona wakati upi magari hayo yatumie barabara za DART.

Amesema zipo nyakati za dharura ambapo magari ya Polisi, zimamoto, gari la wagonjwa ama gari binafsi ambalo ndani yake kabebwa mgonjwa aliyezidia yanapaswa kupewa nafasi ya kupita katika barabara hizo bila kusababisha malumbano

Pamoja na hayo James pia amewataka wananchi kuheshimu matumizi ya miundombinu ya mwendokasi huku akibainisha kuwa asilimia kubwa ya ajali zinazotokea klna kuhusisha mabasi hayo zimesababishwa na wavamiaji.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa DART Dkt. Edwin Mhede amesema wao kama DART jukumu lao ni kuhakikisha wanatoa huduma kwa kiwango cha juu na kwa wakati kwa kutumia Barbara zake hivyo chombo kingine tofauti na mwendokasi kupita katika barabara hizo lazima wakinyoshee kidole kwa kuwa sheria pia imeweka wazi

Aidha alisema ushauri uliotolewa na Mkuu wa Wilaya wao kama DART kwao wanauona mzuri kwa kuwa umelenga kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma bora za mabasi hayo.

Naye Kamanda Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam William Mkonda amesema kazi ya Jeshi la Polisi ni pamoja na kusimamia miundombinu ya DART liweze kufikiwa na hivyo kutimiza adhma ya Serikali ya kuwekeza katika Barabara hizo ili ziweze kupitika kwa urahisi muda wote kwa magari maalumu.

Amesema kwa wale wachache ambao dhana ya utii wa Sheria bila shuruti kwao bado tatizo, Jeshi hilo linawashughulikia kwa mujibu wa Sheria zilizowekwa za matumizi ya miundombinu hiyo.

Amesema wanashirikiana vizuri na DART kuhakikisha watumiaji wa Barabara hizo wanafuata taratibu zilizowekwa huku akibainisha kuwa kufanyika kwa kikao hicho ni mwanzo mashirikiano na DART kwa ajili ya maendeleo ya mradi huo.

Post a Comment

0 Comments