Ticker

6/recent/ticker-posts

DKT.FRANCIS ATEMBELEA KIWANDA CHA UCHAPISHAJI CHA TET


*********************

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Francis Michael amefanya ziara katika kiwanda cha uchapaji cha Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) cha Press A na katika maghala ya kuhifadhia vitabu yaliyopo katika eneo la EPZA jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu amekagua kazi ya uchapaji wa machapisho mbalimbali inayoendelea kiwandani hapo pamoja na kazi ya usafirishaji wa vitabu vinavyosambazwa kwenda katika halmashauri mbalimbali nchini. 

Katika kuhitimisha ziara yake, Katibu Mkuu ameipongeza TET kwa kazi nzuri inayofanya ya uchapaji na usafirishaji wa machapisho mbalimbali.

Aidha, Katibu Mkuu ameiagiza TET kuandika maandiko yatakayoiwezesha kupata fedha za kununua mashine za kisasa na zenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi ya uchapaji pamoja na kujenga ghala kubwa la kuhifadhia machapisho.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt.Aneth Komba amemshukuru Katibu Mkuu kwa kufanya ziara hiyo na kuifahamu TET na kujionea kazi mbalimbali zinazofanyika na kuahidi kuyafanyia kazi maagizo aliyoyatoa.

Post a Comment

0 Comments