Ticker

6/recent/ticker-posts

IDADI YA VIFO VITOKANAVYO NA MATUMIZI YA KEMIKALI YAFIKIA MILIONI MBILI




***********

Na Magrethy Katengu

Imeelezwa kuwa idadi ya vifo vitokananvyo na matumizi ya kemikali imeongezeka hadi kufikia milioni mbili kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa 2019 na Shirika la afya Duniani (WHO) hivyo lazima juhudi za makusudi zifanyike kudhibiti .

Akizungumza Jijini Dar es Sala Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt Fidelice Mafumiko wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ambayo yameandaliwa na shirika la umoja wa kimataifa linalohusika na utafiti kwa kushirikiana na ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali ya Tanzania ambapo amesema madhara ya matumizi ya kemikaki yanaongezeka.

" Kila mwaka Shirika la afya Duniani WHO limetoa takwimu zikionyesha idadi ya vifo vinaongezeka kwani 2012 vilikuwa milioni moja nukta tatu,.2016 vilikuwa milioni moja laki sita huku 2019 vikiwa ni milioni mbili hivyo kama Tanzania tunatoa Elimu kwa wadau namna bora ya kudhibiti kemikali isiathiri afya zao"amesema Mkemia Mkuu

Mkemia Mkuu Dkt Mafumiko mesema kuwa idadi ya vifo vitokanavyo na matumizi ya kemikali hatarishi hadi kufika mwaka 2019 ilifikia watu milion mbili inaweza kuongezeka maradufu endapo elimu haitaendelea kutolewa.

Dkt Mafumiko amesema kuwa mafunzo hayo yameleta chachu kubwa kwani wataalamu wa serikali pamoja na sekta binafsi walikutanishwa kwa pamoja kuweza kupatiwa elimu pana namna yakuepukana na matumizi ya kemikali hatarishi kwa binadamu na mazingira.

“Ofisi yangu imeshirikiana na shirika la umoja wa kimataifa linalohusiana na tafiti kufanya mafunzo haya ya mfumo wa kidunia wa kufuatilia usafirishaji wa kemikali kutoka zinapozalishwa hadi kwa watumiaji pamoja na kuwa na alama za utambuzi wa kemikali hizo ili kuwezesha kuepikana na madhara yatokanayo na kemikali hizo ikiwemo vifo” amesema Dkt Fidelice Mafumiko 

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo afisa Sera Mazingira ya Biashara kutoka shirikisho la Viwanda Nchini CTI Anna Kimaro ameshukuru kupata semina hiyo ya mafunzo hayo kwani inakwenda kuwasaidia kuchukua tahadhari ya matumizi ya kemikali hatarishi kwenye maneo yao ya kazi.




“Wanachama wetu ndio watumiaji wakubwa wa kemikali, kwani wengi wana Viwanda vikubwa na vidogo wengine wanafanya biashara ya kusafirisha kemikali haya tuliyopata yatatusaidia kuondoa madhara ya kemikali kwenye viwanda hivyo tutatumia alama za utambuzi wa kemikali hizo” amesema Anna.

Post a Comment

0 Comments