Ticker

6/recent/ticker-posts

JESHI LA POLISI LATOKOMEZA PANYAROAD BUGURUNI KISIWANI(GANA) WILAYA YA ILALA.

Pichani ni Mstahiki Meya Wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbulamoto akihutubia katika Mkutano wa hadhara ulofanyika katika Shule ya Sekondari Gana Buguruni Mtaa wa Kisiwani.
Mwananchi Asha Ramadhani akitoa maoni yake juu ya Panya road
Mastahiki Meya Omary Kumbilamoto akimkabidhi barua kutoka kwa Wananchi wa Kisiwani akamfikishie IGP Kamiliisi Wambura

***********************


Na Magrethy Katengu

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mh Omary Kumbilamoto amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kudhibiti kikundi cha wahalifu kijulikanacho kama panya road kwa kurudisha hali ya utulivu ambayo ili potea katika maeneo ya Buguruni Kisiwani(Ghana) ambapo wananchi walikuwa wakiishi kwa wasiwasi.

Pongezi hizo zimelitolewa Jijini Dar es salaam wakati akihutubia Mkutano wa hadhara uliofanyika shule ya Sekondari Gana mtaa wa Kisiwani ambapo amesema juhudi zilizofanywa na ulinzi shirikishi pamoja na Jeshi la Polisi hivyo wananchi wanaweza kutembea na kuishi kwa amani kwani panyaroad wameshadhibitiwa.

"Kipekee nimshuru sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Amos Makala pamoja na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Jumanne Murilo kwakweli wamefanya kazi kubwa sana ilifikia mahala ndugu zetu Waislam walikuwa hawawezi kwenda kuswali swala ya alfajiri sababu ya kuhofia panya road na Wakristo vilevile walikuwa hawawezi kuwahi ibada ya asubuhi sababu ya kuhifia usalama wao" amesema Kumbilamoto.

Pia Diwani wa Kata ya Buguruni Mh Busoro Pazi aliwataka wananchi kutengeneza mazingira ya usalama majumbani kwa kuweka taa nje ya nyumba ambayo itasaidia ulinzi kuweza kumulika mazingira ya nyumba yake.

"Ulinzi shirikishi tusaidiane kuzibaini nyumba zote ambazo hazijawekwa taa nje kwa ajili ya usalama nazo ziweze kuwekwa taa mara moja kwa ajili ya kuhakikisha usalama na kuondoa giza" alisema Pazi.

Sanjari na hayo Mtendaji wa Mtaa wa Kisiwani Mh Azizi Shididi alisema wanajua jitihada wanazozifanya Jeshi la Polisi katika kupambana na panya road kwa hivyo wanalipongeza sana kupitia Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Wambura.

"Licha ya jitihada hizi za jeshi la Polisi linatambua kuna watu wanafanya mikakati ya kulikatisha tamaa jeshi hatua zake linalochukua kuwakabili panya road hivyo niwaombe ma wananchi wa Buguruni Kisiwani kutoa ushirikiano bila kukatishwa tamaa kwakuwa wengi wanaobeza hili zoezi sio wahanga wa panya road" amesema Shididi.

" Mtaa huu wa Ghana wananchi tumeteseka sana na vijana hao wadogo hivyo ni budi kurudisha shukrani kwa jitihada iliyofanyika chini ya Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Kamilius Wambura ...

"Kwa kweli nikiri kwamba pamoja na kuwa na ulinzi shirikishi hatukuwa peke yetu askari nao nilikuwa nao nazunguka usiku mzima na kuwakamata vijana hao huku wengine wakikimbia kusikojulikana na bado tunaendelea kuwasaka "amesema Bakari

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kisiwani Awesu Bakari amesema hali ilikuwa si shwari hapo awali kwani iliwalazimu wananchi Ikifika saa kumi na mbili watu walikuwa wanaacha shughuli zao kujifungua ndani lakini bado walivamiwa takribani nyumba zilivunjwa na kuporwa mali zao lakini Jeshi lilikuwa halilali usiku na mchana hali Sasa ni shwari .

Uwesu Bakari aliwataka wazazi kushirikiana na jeshi la polisi endapo mzazi atabaini mtoto wake amekamatwa kwa tuhuma za uhalifu aweze kumuacha kwanza ajifinze maadili na sio kukimbilia kumtolea zamana ambapo wakirudi mtaani wanarudia sababu hawajakaa kwa muda mrefu ili abadilishe tabia.

"Namshukuru sana Polisi Kata vijiwe vyote hapa anaingia lakini mtu akikamatwa dakika mbili mzazi anaenda kituoni kwenda kumtoa kwa kufanya hivi Jeshi la Polisi munalivunja nguvu muache akae kwani asiyefunzwa na mamae hufunzwa na ulimwengu" amesema Uwesu.

Kwa upande wake mwananchi ASha Ramadhani amesema hawana namna wanalishukuru Jeshi lakini anasema wale waliowaficha vijana wao majumbani na wengine wamewatorosha watawataja huku wakionekana wanafanya uhalifu watawakamata kwa mikono yao kwani wamechoka kwani

Vilevile Mwananchi wa Mtaa huo wa Kisiwani aliejitambulisha kwa jina la Prisca Masanja alisema juhudi zisizimike kwani limejirudia kwa mara ya pili hivyo wanashukuru Jeshi la Polisi kwa kuweza kuleta amani katika Mtaa huo na kusema kuwa wale panya road ni wauwaji na kuwataka wazazi ambao wamewaficha watoto wao ndani wawasalimishe kituo cha Polisi .

Naye Abdulimadi Hamisi amesema Wazazi wamezembea kwenye malezi tangu watoto wakiwa wadogo hivyo haya matunda ndiyo wanayoyapata watoto wanafanya vitendo vya uhalifu wanakamatwa na wengine kufia mikononi mwao kwa vipigo vikali hivyo

Aidha wakazi wa Buguruni Kisiwani, Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es salaa, wametuma Salamu maalum kwa Jeshi la Polisi kupitia kwa IGP. Camillius Wambura wakimtaka aendelee na Operesheni za kuwakabili Wahalifu hususani ni Panya Road, ambao wamekua wakihatarisha maisha yao.

Post a Comment

0 Comments