Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKAMANDA WA POLISI WAHAMASISHA UTALII, WAONYA WANAOFANYA UJAGILI


Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Wakuu wa Vikosi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu CP Benedict Wakulyamba (katikati) ambapo kwa pamoja walitembelea hifadhi ya taifa ya Mikumi na kujionea utalii na vivutio vilivyopo kwenye hifadhi hiyo. Kamishna Wakulyamba pia aliwataka wananchi kuendelea kulinda rasilimali za utalii na kutembelea utalii wa ndani. Picha na Demetrius Njimbwi Jeshi la Polisi

**********************

23 OKTOBA 2022 MIKUMI, MOROGORO

Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Wakuu wa Vikosi wamewaonya baadhi ya watu wanaofanya vitendo vya ujagili na kuharibu baadhi ya vivutio mbalimbali vya taifa ambavyo ni urithi wa vizazi vijavyo.

Akiwaongoza kutembelea hifadhi ya taifa ya Mikumi, kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu CP Benedict Wakulyamba amesema kuwa, kufuatia uzinduzi wa filamu ya Royal Tour imesaidia kufunguka kwa utalii nchini ambapo watu mbalimbali wamekuwa wakitembelea hifadhi pamoja na vivutio vilivyopo.

Aidha, kamishna Wakulyamba, amewataka wananchi na Watanzania kwa ujumla kuendelea kulinda rasilimalia za taifa pamoja na kutembelea na kufanya utalii wa ndani.

Naye Bi. Liz Wachuka, ambaye ni muwezeshaji wa warsha ya kuwajengea uwezo wa mawasiliano ya kimkakati na uongozi Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Wakuu wa Vikosi amesema kuwa, jamii inapaswa kutambua kazi waliyonayo Maafisa wa Polisi katika kulinda usalama wa raia na mali zao.

Kwa upande wake Mhifadhi wa hifadhi ya Mikumi Bwana Goodluck Minja amesema kuwa, Wadau mbalimbali wamekuwa wakitembelea hifadhi hiyo hivyo ziara ya Makamanda wa Polisi itasaidia kuwezesha kuutangaza utalii pamoja na vivutio vilivyopo kwenye hifadhi ya Mikumi.

Post a Comment

0 Comments