Ticker

6/recent/ticker-posts

NSSF SINGIDA YAKAMILISHA MAANDALIZI WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA DUNIANI

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Singida, Oscar Kalimilwa akizungumzia maandalizi ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani ambapo kilele chake ni Octoba 7, 2022.
Kazi zikiendelea ofisi za mfuko huo.
Kazi ikiendelea.
Muonekano wa maandalizi kuelekea kilele cha wiki hiyo.

Dotto Mwaibale na Philemon Mazalla Singida

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Singida umekamilisha maandalizi ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani ambapo kilele chake ni Octoba 7, 2022 siku ya Ijumaa.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Meneja wa NSSF Mkoa wa Singida, Oscar Kalimilwa alisema na wao wanaadhimisha siku hiyo kuonesha kuwajali wateja wao chini ya kauli mbiu isemayo ‘Huduma bora ndio kipaumbele chetu’

Alisema katika maadhimisho hayo wameandaa baadhi ya shughuli ambazo watazifanya siku hiyo ya kilele ambapo watachangia damu, kutoa msaada wa vitu mbalimbali Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida ya Mandewa.

Alisema siku hiyo ya kilele wameandaa keki maalumu ambayo itakatwa na wataila pamoja na wateja wao ikiwa ni ishara ya kuwathamini kwani ndio wanaowafanya waendelee kuwepo na kuwa wamejipanga vilivyo kuifanya siku hiyo kuwa ya mafanikio kwao na wanachama wao.

Aidha Kalimilwa alisema wataitumia siku hiyo kutoa elimu kwa wanachama ambao hawana elimu kuhusu mifuko hiyo ya jamii na akatoa wito kwa wananchi na wanachama wao waendelee kuiamini NSSF kwani kuwepo kwake kunasaidia kupambana na majanga yanayomtokea binadamu.

Post a Comment

0 Comments