Ticker

6/recent/ticker-posts

SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN LAKABIDHI MIONGOZO, UGAWAJI CHAKULA SHULENI.



***************************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.


JUMLA ya watumishi 40, wakiwemo walimu 24 wa shuke za msingi katika Wilaya za Handeni na Mkinga mkoani Tanga wamekabidhiwa miongozo ya utoaji wa chakula shuleni kupitia mpango wa Taifa wa ugawaji huo.

Shirika lisilo la Kiserikali la Save the Children Mkoa wa Tanga limekabidhi miongozo hiyo kupitia mpango huo ambao unawagusa wanafunzi zaidi ya 28, 110 wa shule za msingi 53 katika Wilaya hizo mbili ambazo zilionekana kukabiliwa na uhaba wa chakula katika tathimini ya lishe nchini.

Akiongea wakati wa makabidhiano hayo, Mratibu wa Uhakika wa Chakula Mkoa wa Tanga Anania Yusto amesema miongozo iliyozinduliwa itakwenda kusimamia na kuratibu namna gani viongozi wa shule watakavyo lisha shule zao.

Yusto amebainisha kwamba wao kama viongozi wa Shirika la Save the Children kupitia mradi wao wa uhakika wa chakula ambao wanashiriliana na Shirika la World Vision kazi yao kubwa ni kuhakikisha miongozo hiyo inadhibitiwa.

"Lakini pia tunaratibu zoezi zima la hii miongozo na kuendelea kusimamia matumizi yake huko mashuleni, kwahiyo hii miongozo itakwenda kuhakikisha shule hizi 53 zinazopata chakula kupitia mradi wetu, unaendelea kupata miongozo na rejea" amesema.

Aidha amebainisha kwamba mradi huo pia imeweka wigo mpana kwa katika utendaji wake kwani pia wanakabiliana na majanga mbalimbali ambayo yametokana na mvua iliyosababisha ukosefu wa chakula.


"Na kwa tukio hilo, tutahakikisha tunaendelea kuratibu hali halisi ya vijana wetu walioko mashuleni kupitia miongozo itakayotolewa huko mbele za upimaji wa hali ya lishe itakayotolewa mashuleni" amesema.


Nao walimu waliokabidhiwa miongozo hiyo wamesema mradi huo umesaidia kuondoka utoro kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kupunguza kwa kiasi kikubwa mimba za utotoni kwakuwa watoto hakiingia shule asubuhi wanarudi jioni wakiwa wameshiba hivyo kuepuka vishawishi vingi.


"Idadi ya watoto imeongezeka kwa kiasi kikubwa shuleni, na hata utoro hakuna kwakuwa inapofika muda wa kwenda kula watoto hawaendi majumbani wanabaki shuleni, huu mradi umetusaidia sana sisi walimu na hata watoto wetu" amesema Grace Mbanga, Ofisa elimu Sayansikimu, halmashauri ya Wilaya ya Handeni.


Mwalimu Elibariki Samballu amesema mpango huo kabambe umekuwa mzuri kutokana na matokeo mazuri kwa sababu wameweza kuchochea kiwango cha mahudhurio ya wanafunzi.


"Wengine ambao walikuwa na utoro wa rejareja kupitia mradi huu wamerudi na wamekuwa na muitikio mkubwa, kuanzia darasa la awali hadi la saba wameweza kufika shule kwa wakati, zamani wengi wao walikumbwa na matatizo mbalimbali ukifika muda wa kwenda majumbani kupata chakula hasa kwa wale wanayoishi mbali na shule"

Post a Comment

0 Comments