Ticker

6/recent/ticker-posts

SHULE YA MSINGI MUMTAZ YAIBUKA KIDEDEA UFAULU MTIHANI WA DINI YA KIISLAM

Amiri wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania,Sheikh Mussa Yusuph Kundecha (katikati),akitangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba wa elimu ya dini ya kiislamu uliofanyika Septemba 14,mwaka huu.Kulia ni mwenyekiti wa taasisi ya Taasisi ya Islamic Education Panel.Mpigapicha


**************************

Na Magrethy Katengu

Jopo la wataalamu wa elimu ya limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba wa elimu ya dini ya kiislamu uliofanyika septemba 14,2022 na kusema kuwa jumla ya shule 3710 katika mikoa 25 na halmashauri 151 zilishiriki kufanya mtihani huo huku shule ya Mumtaz iliyopo Mwanza imeibuka kidedea

Akizungumzia na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati wa kutangaza matokeo hayo Amiri wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Mussa Yusuph Kundecha, wakati akitangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba wa elimu ya dini ya kiislamu uliofanyika Septemba 14, mwaka huu iliyo chini ya taasisi ya Taasisi ya Islamic Education Panel amesema kuwa jumla ya watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 163,143 na waliofanya mtihani ni 142,522 sawa na asilimia 87.36

Shekh Kundecha amesema kuwa idadi ya watahimiwa ambao hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali ni 20621huku idadi ya watahiniwa waliofaulu kwa kupataadaraja A hadi C ni 95,166 sawa na asilimia 66.77 ya watahiniwa wote 142522 idadi ya watahiniwa waliopata madaraja ya D na E ni 47,356 sawa na asilimia 33.23 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani.

"Watahiniwa na madaraja yao ni kama ifuatavyo waliopata daraja la kwanza (A) ni wanafunzi 3,567,daraja la pili (B) ni wanafunzi 22,587,daraja la tatu (C)ni 69,012,daraja la nne (D)45,781 huku.daraja la mwisho (E) ikiwa ni 15,575"amesema mjumbe huyo IEP

Sanjari na hayo amezitaja shule 10 bora katika la shule zenye watahiniwa 20 na kuendelea,Sheikh kuwa ni Mumtaz (Mwanza),Istiqaama(Tabora),Rahma (Dodoma),Algebra Islamic(Dar es salaam),Dumila(Morogoro)Islamiya(Mwanza)Hedaru (Kilimanjaro),Daarul Arqaam(Dar es salaam),Mbagala Islami(Dar es salaam pamoja na Maarifa Islamic (Dar es salaam)

Sambamba na hayo amesema kuwa shule 10 za mwisho zilizopata ufaulu mdogo kabisa ni pamoja na shule za msingi Kilimani (Ilala),Mwasenga(Kigoma Ujiji),Umoja (Tabora),Bugoyi (Shinyanga),Mvuti(Dar es salaam)Kasamwa(Geita),Muzdalifa Islamic(Lindi),Mawala (Kilimanjaro)Sipungu (Tabora)pamoja na Izumangabo (Geita).

Pia alizitaja halmashauri 10 bora ni ambapo ikiongozwa na Hamashauri ya Wilaya ya Songea (Ruvuma), Mji wa Newala (Mtwara),Ngorogoro (Arusha),Ukerewe (Mwanza),Kalambo (Rukwa),Newala (Mtwara),Tunduma (Songwe),Mafia (Pwani), Mkuranga (Pwani) na Mji Nzega (Tabora).

Post a Comment

0 Comments