Ticker

6/recent/ticker-posts

TANZANIA MGUU SAWA KUIKABILI UFARANSA


********************

Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 17 (Serengeti Girls) jioni ya Oktoba 14, 2022 wamefanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wao na Ufaransa utakaochezwa saa 4: 30 jioni saa za nchini India, Oktoba 15 Uwanja wa Pandit Jawaharlal Nehru jijini Goa.

Baada ya Mazoezi Kocha wa timu Bakari Shime ameeleza kuwa hali ya wachezaji iko vizuri, morali ya kupambana ipo kwa ajili ya taifa.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa ( BMT) ameshuhudia mazoezi hayo na kusema wachezaji wana ari, na mazoezi wamefanya vizuri na wanaoenakana wako tayari kuikabili Ufaransa na baadae mechi dhidi ya Canada.

Post a Comment

0 Comments