Ticker

6/recent/ticker-posts

TEA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU YA WATU WAZIMA

Mnufaika wa SDF katika sekta ya Uchukuzi akitoa elimu kuhusu matengenezo ya pikipiki na bajaji aliyopata kupitia ruzuku ya SDF.

*****************

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) inashiriki katika maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu wazima katika viwanja vya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam - DUCE kwa lengo la kuonyesha mchango wa Elimu isiyo katika mfumo rasmi kwa jamii.

Maadhimisho hayo yanafanyika sambamba na maonyeho ambapo yameanza rasmi leo Oktoba 17 hadi Oktoba 21.

TEA inashiriki maadhimisho na maonyesho hayo kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) ambao unalenga kutoa mafunzo ya Ujuzi na Stadi za Kazi katika sekta sita za kipaumbele ambazo ni Ujenzi, Utalii na Huduma za Ukarimu, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Kilimo na Kilimo Biashara, Uchukuzi pamoja na Nishati.

Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) ni sehemu ya Programu ya Kuendeleza Elimu ya Ujuzi na Mafunzo ya Stadi za Kazi zenye kuleta Tija katika Ajira (ESPJ) na Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Kukuza na Kuendeleza ujuzi nchini (NSDS) chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambayo inasimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na inafadhiliwa na Serikali pamoja na Benki ya Dunia (WB)

Zaidi ya wananchi 36,870 wamenufaika na ruzuku ya Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi ili kuwawezesha kuajiriwa au kujiajiri wenyewe. Awamu ya kwanza ya SDF ilianza kutekelezwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo Taasisi 15 zilifadhiliwa kwa jumla ya Shilingi Bilioni 3.1 wakati katika awamu ya pili Taasisi 81 zimenufaika kwa ufadhili wa kiasi cha Shilingi Bilioni 9.7 zikitumika kuendesha programu za mafunzo ya ujuzi.

Post a Comment

0 Comments