Ticker

6/recent/ticker-posts

WABUNGE WAPYA WA BUNGE LA AFRIKA WAAPISHWA..WAMO KUTOKA TANZANIA


Wabunge kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Mhe. Anatropia Theonest, Mhe. Toufiq Salim Turkey na Mhe. Ng’wasi Damas Kamani wakila kiapo kuwa wabunge wa Bunge la Afrika wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kwanza cha Kawaida cha Bunge la Sita la Afrika

Na Kadama Malunde - Midrand Afrika Kusini
Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament – PAP) Mhe. Chief Fortune Charumbira amefungua Kikao cha Kwanza cha Kawaida cha Bunge la Sita la Afrika huku Wabunge Wabunge 11 kutoka Burundi, Morocco, Msumbiji, Somalia na Tanzania wakiapishwa kuwa Wabunge wa Bunge la Afrika (PAP).

Mkutano huo wa Bunge unafanyika katika Makao Makuu ya Bunge la Afrika Midrand Johannesburg Afrika Kusini ukiongozwa na Kauli Mbiu ya Umoja wa Afrika ya Mwaka 2022 “Kujenga Uthabiti kwenye Lishe katika Bara la Afrika : Kuongeza mtaji wa watu, maendeleo ya kijamii na kiuchumi”.

Wabunge wapya wa Bunge la Afrika waliokula kiapo ni Mhe. Anatropia Theonest, Mhe. Toufiq Salim Turkey na Mhe. Ng’wasi Damas Kamani kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Bernardine Nduwomana(Burundi) , Mhe. Hannaa Benkhair (Morocco) Mhe. Sarfina Filipe Franco Chindaculema (Msumbiji) , Mhe. Seneta Prof. Abdi Ismael Samatar, Mhe. Mohamed Jamal Mursal, Mhe. Abdulrahman Mohamed Hussein, Mhe. Aden Mohamed Nur na Mhe. Zamzam Muhumed Omar (Somalia).
Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament – PAP) Mhe. Chief Fortune Charumbira akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kwanza cha Kawaida cha Bunge la Sita la Afrika leo Jumatatu Oktoba 31,2022 katika Makao Makuu ya Bunge la Afrika, Midrand Afrika Kusini. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament – PAP) Mhe. Chief Fortune Charumbira akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kwanza cha Kawaida cha Bunge la Sita la Afrika leo Jumatatu Oktoba 31,2022 katika Makao Makuu ya Bunge la Afrika, Midrand Afrika Kusini. 
Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament – PAP) Mhe. Chief Fortune Charumbira (kulia) akiongoza Kikao cha Kwanza cha Kawaida cha Bunge la Sita la Afrika leo Jumatatu Oktoba 31,2022 katika Makao Makuu ya Bunge la Afrika, Midrand Afrika Kusini. 
Wabunge kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Mhe. Anatropia Theonest, Mhe. Toufiq Salim Turkey na Mhe. Ng’wasi Damas Kamani wakila kiapo kuwa Wabunge wa Bunge la Afrika wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kwanza cha Kawaida cha Bunge la Sita la Afrika
Wabunge kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Mhe. Anatropia Theonest, Mhe. Toufiq Salim Turkey na Mhe. Ng’wasi Damas Kamani wakila kiapo kuwa Wabunge wa Bunge la Afrika wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kwanza cha Kawaida cha Bunge la Sita la Afrika
Mhe. Bernardine Nduwomana kutoka nchini Burundi akila kiapo kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika leo wakati wa  ufunguzi wa Kikao cha Kwanza cha Kawaida cha Bunge la Sita la Afrika (PAP).
Mhe. Hannaa Benkhair kutoka nchini Morocco akila kiapo kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kwanza cha Kawaida cha Bunge la Sita la Afrika
Mhe. Sarfina Filipe Franco Chindaculema kutoka Msumbiji  akila kiapo kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kwanza cha Kawaida cha Bunge la Sita la Afrika
Wabunge kutoka Somalia ambao ni Mhe. Seneta Prof. Abdi Ismael Samatar, Mhe. Mohamed Jamal Mursal, Mhe. Abdulrahman Mohamed Hussein, Mhe. Aden Mohamed Nur na Mhe. Zamzam Muhumed Omar  wakila kiapo kuwa wabunge wa Bunge la Afrika wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kwanza cha Kawaida cha Bunge la Sita la Afrika
Wabunge kutoka Somalia ambao ni Mhe. Seneta Prof. Abdi Ismael Samatar, Mhe. Mohamed Jamal Mursal, Mhe. Abdulrahman Mohamed Hussein, Mhe. Aden Mohamed Nur na Mhe. Zamzam Muhumed Omar  wakila kiapo kuwa wabunge wa Bunge la Afrika wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kwanza cha Kawaida cha Bunge la Sita la Afrika

Zifuatazo ni picha Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament – PAP) Mhe. Chief Fortune Charumbira akiwakabidhi Bendera ya Bunge la Afrika Wabunge wapya wa Bunge la Afrika (PAP)

Post a Comment

0 Comments