Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI BASHE ASISITIZA MWAMKO WA USAJILI KWA WAKULIMA

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akizungumza na wanachama wa SACCOS kutoka sehemu mbalimbali katika maadhimisho ya siku ya Ushirika wa Akiba na Mikopo Duniani yaliyofanyika Oktoba 17,2022 kwenye Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mhe.Hassan Masala akizungumza na wanachama wa SACCOS kutoka sehemu mbalimbali kwenye Maadhimisho ya Siku ya Ushirika wa Akiba na Mikopo Duniani(ICUD 2022) yanayofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Furahisha mkoani Mwanza yenye kauli mbiu isemayo imarisha uwezo wa kifedha wa siku zijazo kupitia ushirika wa akiba na mikopo.
Mrajis wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Akiba na Mikopo, Dk Benson Ndiaye akizungumza nachama wa SACCOS kutoka sehemu mbalimbali kwenye Maadhimisho ya Siku ya Ushirika wa Akiba na Mikopo Duniani(ICUD 2022) yanayofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Furahisha mkoani Mwanza yenye kauli mbiu isemayo imarisha uwezo wa kifedha wa siku zijazo kupitia ushirika wa akiba na mikopo.

Wanachama wa Saccos kutoka sehemu mbalimbali wakimsikiliza Waziri Hussein Bashe wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya ushirika wa akiba na mikopo duniani (ICUD 2022) yanayofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Furahisha mkoani Mwanza.


***************

Na Sheila Katikula, Mwanza

Serikali imewataka wakulima kujisajili ili waweze kupata namba ya siri ambayo itasaidia kupata fursa ya kununua mbolea ya ruzuku iliyotolewa na serikali.

Hayo yamesemwa Oktoba, 17 na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati akizungumza na wanachama wa Saccos kutoka sehemu mbalimbali kwenye maadhimisho ya siku ya ushirika wa akiba na mikopo duniani yanayofanyika kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.

"Ukijisajili utapewa namba ya siri kwenye simu yako itunze usimpe mtu kwani ukimpa mtu anaweza kununua mbolea kupitia namba hiyo na kupelekea kukosa fursa hiyo. 

"Ukinunua mbolea utapewa ujumbe wa idadi ya mbolea uliyonunua kama ipo tofauti toa taarifa ili serikali iweze kufatilia na kuchukua hatua kwa watu ambao wanaiba mbolea hizo,"amesema Bashe.

Aidha amewataka wakulima kutuma maombi kwenye Wizara ya Kilimo ili waweze kupata fursa ya kuuza mbolea hizo kwenye maeneo yenu Kwa sababu wanamtandao .

Alibainisha hadi hivi sasa kuna changamoto ya mawakala kwenye baadhi ya maeneo na serikali inatambua na ipo hatua ya mwisho kuongeza idadi ili kutatua tatizo hilo ili wakulima waweze kununua mbolea karibu na maeneo yao.

Bashe aliwaomba wakulima kutumia vizuri mvua za mapema pamoja na kuchukua tahadhari ya chakula kwa kuepuka uuzaji holela wa chakula kwani hali ya hewa mwaka huu inaoneka si nzuri.

Naye Mrajis wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Akiba na Mikopo, Dk Benson Ndiaye alimuhakikishia Waziri, Vyama vya Kuweka na Kukopa (SACOSS) zipo hai na zinaendelea kuwa salama ili kukidhi mahitaji ya kifedha Kwa wanachama, wadau na watanzania nchini.

Amesema Saccos zilizopewa leseni 728 zimeendelea kuongeza wanachama kutoka 1,324,513 hadi kufikia wanachama 1,567,201 mwezi septemba 2022 kwani idadi hiyo inajumuisha Saccos 407 ambazo hazijapewa leseni.

Amesema mpaka sasa kwenye vyama vya akiba na kukopa, amana za wanachama zimeongezeka kutoka sh bilioni 678.1 mwaka 2021 hadi kufikia sh Bilion 709.67 kufikia septemba mwaka huu.MWISHO

Post a Comment

0 Comments