Ticker

6/recent/ticker-posts

BINURU AKANUSHA UWEPO WA SHULE ZINAZOTUMIKA KAMA MADANGULO SENGEREMA
*************************

Na SHEILA KATIKULA,MWANZA

Mkurungenzi wa halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, Binuru Shekidele amekanusha kuwepo kwa shule zinazotumika kama madangulo .

Ametoa taarifa hiyo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake amesema hivi karibuni kuna baadhi ya vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii viliandika habari za uongo kuwepo kwa vyumba vya madarasa vinavyotumika kama dagulo katika halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani mwanza.

Aidha , Shekidele amesema kuwa picha za shule iliyotajwa katika mitandao ya kijamii pamoja na chombo cha kuchapisha habari hapa nchi siyo za kweli na kuwaomba wadau na wa habari kuzipuuza taarifa hizo.

“ Ndugu waandishi wa habari katika baraza la madiwani kuliibuka hoja ya fedha za kapitesheni kifungu cha asilimia 30 ya fedha ya ukarabati na nililitolea ufafanuzi kuwa kuna baadhi ya shule zilikuwa na changamo ya milango lakini kwa sasa hakuna shule yenye changamoto ya milango na madilisha kwani muda wa shule ukiisha madarasa yanafungwa “ amesema Shekidele.

"Nawaomba waandishi wa habari muwemna kufatilia taarifa kwa usahihi kabla ya kuuhabarisha umma ili kuondoa maswali kwa wananchi kwani habari hii imeposha jamii.

Post a Comment

0 Comments