Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI RAFIKI WA MAJI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipanda mti kuashiria kuzindua rasmi kampeni ya kitaifa ya upandaji miti rafiki wa maji kwenye vyanzo vya maji, zoezi lililofanyika katika chanzo cha maji cha Nzovwe 1 kata ya Mwakibete Jijini Mbeya leo tarehe 16 Novemba 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akifungua kitambaa maalum kuashiria kuzindua rasmi kampeni ya kitaifa ya upandaji miti rafiki wa maji kwenye vyanzo vya maji, mara baada ya kupanda mti katika chanzo cha maji cha Nzovwe 1 kata ya Mwakibete Jijini Mbeya leo tarehe 16 Novemba 2022. (Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selamani Jafo, Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson kulia ni Waziri wa Maji Jumaa Aweso na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Jiji la Mbeya mara baada ya kuzindua rasmi kampeni ya kitaifa ya upandaji miti rafiki wa maji kwenye vyanzo vya maji, zoezi lililofanyika katika chanzo cha maji cha Nzovwe 1 kata ya Mwakibete Jijini Mbeya leo tarehe 16 Novemba 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na Kamishna wa Uhifadhi Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Prof Dos santos Silayo juu ya kuhakikisha wanazalisha miche ya kutosha ya miti rafiki wa maji kwaajili ya upandaji wa miti hiyo nchi nzima wakati wa kuzindua rasmi kampeni ya kitaifa ya upandaji miti rafiki wa maji kwenye vyanzo vya maji, zoezi lililofanyika katika chanzo cha maji cha Nzovwe 1 kata ya Mwakibete Jijini Mbeya leo tarehe 16 Novemba 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia viongozi na wadau wa sekta ya maji nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa nane wa mwaka wa bodi za maji za mabonde unaofanyika Jijini Mbeya. Tarehe 16 Novemba 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizindua Mpango wa uhifadhi wa vyanzo vya maji mara baada ya kufungua mkutano mkuu wa nane wa mwaka wa bodi za maji za mabonde unaofanyika Jijini Mbeya. Tarehe 16 Novemba 2022. (Kushoto ni Waziri wa Maji Jumaa Aweso na kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selamani Jafo)

Post a Comment

0 Comments