Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAIPONGEZA UDSM KUENDELEA KUIBUA TAFITI ZINAZOSAIDIA KUTENGENEZA SERA


*********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imekipongeza Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kwa kuendelea kuja na tafiti mbalimbali zinazoisaidia Serikali katika utengenezaji wa sera za Kitaifa.

Pongezi hizo amezitoa leo Novemba 22,2022 Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt.Khatibu Kazungu katika warsha ya Shule Kuu ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Amesema Serikali inathamini kwa kiasi kikubwa michango ya tafiti inayofanywa na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kwani inasaidia katika utengenezaji wa sera ambazo Serikali inazitumia katika kuendeleza shughuli mbalimbali za kitaifa nchini.

Nae Mwakilishi wa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Utafiti, Prof.Neema Mori amesema kuwa chuo kimeandaa warsha hiyo ili kuwasilisha machapisho ya tafiti mbalimbali yaliyo andaliwa na chuo hicho na cha Copenhagen ambapo katika tafiti hizo wameangalia namna nchi ya Tanzania ilivyopitia maboresho katika kukuza uchumi.

Kwa upande wake Mtafiti Bw. Aikaeli Jehovanis ameishukuru serikali kwa kuona mchango wa watafiti katika kuleta maendeleo ya taifa kwa kusaidia nchi katika utungaji wa sera, pia ameeleza kuwa tafiti hizo zimeandaliwa na watafiti wakubwa na wadogo,

Post a Comment

0 Comments