Ticker

6/recent/ticker-posts

UDSM YAWAKUTANISHA WADAU WA TAFITI KATIKA KONGAMANO LA KITAIFA LA SAUTI YA SAYANSI YA JAMII


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Wanataaluma wa Sayansi za Jamii wamesema mabadiliko yanayoendelea kutokea duniani na athari zake hususani kusini mwa Dunia yanaweza kudhibitiwa endapo wataalam watazingatia kuielewa na kushirikiana na jamii katika mambo wanayofanya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 10,2022 Jijini Dar es Salaam katika kongamano la Kitaifa la Sauti ya Sayansi ya Jamii lililoandaliwa na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Utafiti, Prof. Bernadeta Killian amesema fani ya Sayansi za Jamii zinaumuhimu mkubwa katika maendeleo ya jamii kwasababu ndio yanatoa majibu kwa masuala mbalimbali yanayoendelea kwenye jamii inayotuzunguka.

Amesema mara nyingi fedha za utafiti hutolewa kwenye masuala ya teknolojia, uhandisi na masuala mengineo kuliko kwenye fani ya sayansi jamii ambayo imekuwa muhimili mkubwa katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii inayotuzunguka.

Nae Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Christine Noel amesema wamekuwa wakishirikiana na wenzao wa vyuo vingi duniani kuhusiana na tafiti ambazo zinahusu maisha ya watu kiasiasa, kiuchumi, kitamaduni na namna zote za kijamii.

Amesema kila baada ya miaka miwili wanakuwa na mkutano ambao wanawaleta wenzao na kujadili na kuchakata taarifa zao za kitafiti alafu wanaona namna ya kutoa muongozo wa kitaaluma na namna ya kushauri sera za Serikali.

Aidha amesema kupitia majadiliano hayo na wenzao kutoka mataifa mbalimbali wanapata uelewa mpana zaidi na kuweza kufundisha vizuri zaidi kwenye jamii.

Wataalamu wa Sayansi ya jamii kutoka ndani na nje ya bara la Afrika walipata nafasi ya kuwasilisha tafiti walizozifanya zilizoonesha mienendo ya mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwemo tafiti juu ya Janga la UVIKO 19 na maendeleo ya Uchumi wa buluu.

Kongamano hilo lililoongozwa na kauli mbiu isemayo Sayansi ya Jamii na mabadiliko katika nchi za kusini mwa Dunia limeandaliwa na Ndaki ya Sayansi za Jamii ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na hufanyika mara moja baada ya miaka miwili.

Post a Comment

0 Comments