Ticker

6/recent/ticker-posts

FILAMU YA ROYAL TOUR IMELETA MAFANIKIO MAKUBWA HIFADHI YA TAIFA YA MKOMAZI.

Muhifadhi Kiemi akimkabidhi mfuko wenye vipeperushi vya hifadhi, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Sebastian Masanja kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba.
Stanslaus Ngewe akitoa maelezo kuhusu mnyama Nyati ambapo aliwapitisha wageni kwa mnyama huyo.

Muongozo watalii katika hifadhi hiyo Raymond Laban naye akitoa maelezo kuhusu wanyama na tabia zao kwa wageni waliokwenda kufanya utalii.


Mnyama aina ya Faru akiwa malishoni katika mizunguko yake ya kawaida.




Mhifadhi mkuu katika hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Happyness Kiemi akitoa taarifa ya hifadhi.

Watumishi wa Mkoa wa Tanga wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwasili hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.


*******************
Na Hamida Kamchalla, TANGA.


BAADA ya kuzinduliwa filamu ya Royal Tours, hifadhi ya Taifa ya Mkomazi imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuongeza watalii wa nje na ndani na kufanya ongezeko la mapato kwa zaidi ya asilimia 100 katika kipindi cha mwaka 2021/22.


Happyness Kiemi ambaye ni muhifadhi mkuu katika hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ameyasema hayo katika hifadhi hiyo wakati alipotembelea na watumishi wa Mkoa wa Tanga na kusema wanaishukutu serikali kwa kubuni na kuanzishwa filamu ya Royal Tours nchini kwani itaongeza pato la Taifa.


Kiemi pia amebainisha kwamba watalii wengi wameongezeka kufuatia filamu hiyo ambapo katika kipindi cha nusu mwaka wameweza kuingiza watalii zaidi na kupita kiwango cha mwaka mzima wa 2021 na kwamba watu wengi wameamua kumuunga mkono Rais Samia Sulluhu Hassan katika filamu ya Royal Tours.


"Mwamko wa watalii hapa hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ni mkubwa sana kwa sababu tangu kuzinduliwa filamu ya Royal Tours tumekuwa tukipokea wageni kila siku, tuseme wameongezeka na tumeingiza napata zaidi ya asilimia 100,


"Tunamshukuru sana Muheshimiwa Rais kwa kufanya filamu hii ambayo ndani ya kipindi cha miezi sita tu tumeweza kuingiza mapato zaidi ya mwaka mzima uliopita, hii filamu imeleta manufaa makubwa kwetu Watanzania kwakuwa tunaamini itaongeza zaidi pato la Taifa" amesema Kiemi.


Aidha ameiomba serikali ya Mkoa wa Tanga kuwapa ushirikiano katika kukamilisha ujenzi wa malango mawili yaliyopo eneo la Umba wilayani Mkinga na eneo la Mnazi wilayani Lushoto ambayo yatakapokamilika yatarahishisha shuhuli za utalii lakini pia kuwa rahisi kwa watalii wanaotoka Mkoa wa Tanga kuingia hifadhini.


"Tumeamua kufungua fursa za kiutalii lakini pia kurahisisha watalii wa ndani na nje ya nchi kuingia hifadhini kwa ukaribu zaidi kupitia malango hayo, hii itawahamasisha wananchi wa Mkoa wa Tanga na kuona umuhimu na uwepo wa hifadhi ya Mkomazi " amebainisha.


Naye muongozo watalii Raymond Laban amesema hifadhi hiyo ilianzishwa mwaka 2008 na ukubwa wa kilomita za mraba 3245, na kwamba ina wanyama wa aina tofauti ambao wengine hawapatikani katika hifadhi nyingine nchini.


"Hifadhi yetu ya Taifa ya Mkomazi imejaaliwa kuwa na vivutio vingi sana, wanyama wa aina mbalimbali ambao hawapatikani katika baadhi ya hifadhi nchini wapo hapa, kuna lile kundi la wanyama wakubwa watao, kwamaana ya Tembo, Simba, Nyati, Faru na Chui" amebainisha.


Laban amefafanua kuwa hifadhi Iko katika Mikoa miwali ya Tanga na Kilimanjaro ambapo kwa Mkoa wa Tanga imepakana na Wilaya za Mkinga, Lushoto na Korogwe, na Mkoa wa Kilimanjaro imepakana na Wilaya za Same na Mwanga.


"Lakini pia hifadhi yetu, kwa upande wa kaskazini tumepakana na hifadhi ya Savo ambayo iko nchi jirani ya Kenya, na hii kufanya wanyama kufanya uhamiaji, wanyama wa hifadhi ya Savo wanaingia Mkomazi na vilevile wa Mkomazi kwenda Savo na wanafanya hivi mara kwa mara" ameafanua Laban.


Naye Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Sebastian Masanja alisema lengo la ziara ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ni kuhakikisha kuwa watendaji wa Mkoa wanazifahamu vizuri hifadhi zinazowazunguuka kwa nia ya kuzitangaza na kuhamasisha utalii.


"Moja ya malengo yetu tuliyojiwekea kama Mkoa ni kwamba watendaji wote tuzuunguke na kutembelea hifadhi zetu ambazo zimezunguuka Mkoa wetu tuzijue vizuri lakini pia tuzitangaze ili kuhamasisha utalii na kuongeza pato la Mkoa wetu na Taifa kwa ujumla" amesema.

Post a Comment

0 Comments