Ticker

6/recent/ticker-posts

GPSA YANYAKUA TUZO YA MSHINDI WA TATU YA UANDAAJI HESABU KWA MWAKA 2021


***************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), imeibuka kidedea kwa kushika nafasi ya tatu na kunyakuwa tuzo ya uandaaji hesabu kwa mwaka 2021, Ushindi huo, wameupata katika kipengele cha taasisi za umma. Tuzo hiyo imetolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) Novemba 30,2022 Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu Prof.Geraldine Rasheli amesema ushiriki wa tuzo hizo unawafanya wao kama sekta ya umma wanaandaa hesabu zao kwa mujibu wa taratibu na kanuni zilizoandaliwa kimataifa na zile bodi ambazo zinatambulika nchini.

Lengo lao ni kuwa washindi wa kwanza kwenye mashindano yajayo kwasababu wana timu bora ambayo wamefundishwa na kufundishika na wanautaalamu.

"Tumewekeza kwa wale ambao hawana sifa waweze kufika hapa NBA na kupata mafunzo na kufanya mtihani ili kuweza kuendelea kuboresha timu yetu na kuwa endelevu na kuwa na uhakika wa kuchukua zawadi". Amesema

Post a Comment

0 Comments