Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA USHAURI YA MKOA KAGERA YAHAINISHA MAMBO 11 YATAKAYO KUZA UCHUMI NA MAENDELEO .Na Shemsa Mussa, Kagera.


Kikao cha kamati ya ushauri Mkoa (RCC) kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kilicholenga kujadili ajenda mbalimbali za maendeleo ya Mkoa na utekelezaji wa majukumu ya serikali ,Mkuu wa mkoa wa Kagera Albet Chalamila amesema kwa jitihada za Rais Dkt Samia zimeupa nguvu mkoa huo katika kuendelea kuonekana wa tofauti katika miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na namna anavyoiongoza nchi.

Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe Albert John Chalamila wakati wa kufunga kikao hicho ameyataja mambo muhimu yaliyoafikiwa ndani ya kikao hicho yakatayofanywa ili kukuza mkoa ni pamoja na kuimalisha Ulinzi na usalama wa Mkoa,kutenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda mbalimbali ili kuwavutia watalii na mkoa kuwa na mpangilio mzuri wajengo ,kuomba serikali iwasaidie wamiliki wa vyuo na shule zilizofungwa kutimiza za masharti ili wendelee kufanya kazi na viweze kufunguliwa,


Pia kukuza setka ya utalii kwa ujumla,kuimalisha biashara Mipakani, ujenzi wa stendi ya Magari na uwanja wa ndege,Aidha katika sekta ya elimu kwa mwaka wa fedha 2021/2022 jumla ya shilingi Bilioni 79.5 zimetumika katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.


"Fedha hizo ni nyingi na zinahitaji usimamizi mkubwa hivyo naahidi kuwa tutaendelea kusimamia fedha hizo kwa nidhamu ya juu kwa maslahi ya mkoa na taifa kwa ujumla" alisema Rc Chalamila.


Aidha amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/ 2023 hadi septemba 2022( robo ya kwanza ) tayari mkoa wa Kagera umekwisha pokea shilingi bilioni 21.0 ambapo kati ya fedha hizo nyingi zilikuwa ni kwa ajili ya sekta ya elimu, Afya, pamoja na sekta mbali mbali.


Ameongeza kuwa katika suala la elimu mkoa huo ulipokea Bilioni 17 na milioni 620 kwa ajili ya kutengeneza vyumba vya madarasa 881 na kwa awamu ya pili Bilioni 10 milioni 280 zimetumika kwa ajili ya kujeng madarasa 514 ili kukabiliana na uhaba wa madarasa kwa mwaka 2023.Amesema ujenzi huo wa madarasa umefikia asilimia 85 , Huku akisema dhana ya elimu bila malipo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 mkoa pia ulipokea shilingi bilioni 16.5 kwa ajili ya ada madarasa kwa wakuu wa shule na waratibu elimu kata.

Post a Comment

0 Comments