Ticker

6/recent/ticker-posts

KISHINDO CHA SHAKA UZINDUZI WA KAMPENI JIMBO LA AMANI.


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akimnadi mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Amani Zanzibar, Abdul Yussuf Maalim katika mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za CCM katika uchaguzi huo. (Picha na Fahad Siraj wa CCM)

************************* *



*Asema ni CCM ndiyo yenye uwezo wa kuleta maendeleo ya nchi

*Asisitiza kazi nzuri iliyofanywa na Rais Mwinyi inaonekana Znz

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) amewataka wananchi katika Jimbo la amani kuchagua mgombea iliyemsimamisha kwa kuwa CCM ndiye mwenye uwezo wa kuendeleza wa kuendeleza kazi nzuri ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.

Imesema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amefanya kazi kubwa na nzuri, hivyo anastahili kupewa viongozi watokanao na CCM ili kuendeleza Kasi hiyo.

Aidha, amesema kazi ya kuleta maendeleo hususan katika jimbo hilo haiwezi kuletwa na kila mtu, hivyo kuna kuna umuhimu mkubwa wa kumchagua mgombea aliyesimamishwa na CCM.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Amani, Zanzibar na kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo, Abdul Yussuf Maalim ambaye amesimamishwa na CCM.

"Kazi ya kuleta maendeleo ya nchi hii hapewi kila mtu, kazi ya kuleta maendeleo Jimbo la Amani sio kila mmoja anaweza kuleta maendeleo, wapi wenye uwezo wa kuleta propaganda kwenye jimo la Amani, lakini wapo wenye uwezo wa kuleta maendeleo Wana amani mkasema kweli haya ni maendeleo ambayo tunayahitajia, ndiyo maana tukasema Abdul songa mbele nenda ukapeperushe bendera ya Chama Cha Mapinduzi.

"Ushindi wa CCM katika Jimbo la Amani ni kama kufa na kupona, tutashinda kwa haki, tutashinda kwa amani, lakini tutashinda tukiwa wamoja na tumeshikamana," alisema.

Alisema kazi nzuri iliyofanywa na Rais Samia katika kipindi cha miaka miwili ni kubwa hivyo anastahili kupongezwa na juungwa mkono ikiwamo kumchagulia wagonbea watokanao na CCM.

"Ndani ya kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Dk. Mwinyi mtu apende asipende, afurahi asifurahi Dk. Mwinyi ameupiga mwingi (amefanya vizuri kuleta maendeleo). Mabadiliko tunayoyashuhudia Zanzibar...lazima tukubali matarajio ya wazanzibari kwa Dk. Mwinyi ni makubwa zaidi," alisema.

Kwa upande wake mgombea huyo, alisema iwapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo amejipanga kuendeleza Kasi ya maendeleo kwa kushirikiana na Rais Dk. Mwinyi na viongozi wengine wa Chama, serikali na wananchi kwa ujumla.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Desemba 17, mwaka huu kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Maalim Mussa.

Post a Comment

0 Comments